Katibu Mkuu Chama cha Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi (kushoto) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya mashindano ya Kitaifa ya mchezo wa baseball yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni katika shule ya Sekondari ya Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari na Kutoka kulia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga.
Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mashindano ya mchezo wa Baseball yanayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 na 23 mwezi huu katika shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi na anayemfuatia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga.
Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (katikati) akitoa maelekezo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya namna mchezo wa Baseball unavyochezwa. Kushoto ni Mkufunzi wa mchezo huo Bi. Hellen Prosper Stima na kutoka kulia ni Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Richard Mganga akifuatiwa na Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa Baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi.
Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa Baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari (katikati) akimvalisha Mkufunzi Bi. Hellen Prosper Stima (kushoto) kifaa maalum cha kujikinga wakati wa kucheza mchezo wa baseball. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Chama cha mchezo wa baseball Tanzania (TABSA) Alpherio Nchimbi.
Afisa Michezo Baraza la Michezo Tanzania (BMT) (kushoto) Richard Mganga akiwaeleza waandishi wa habari juu ya mashindano ya mchezo wa baseball yanayotarajiwa kufanyika siku ya tarehe 22 na 23 katika shule ya Sekondari ya Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Marafiki wa mchezo wa baseball Africa (AFAB) Shinya Tomonari.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
Jamani Baseball na sisi wapi na wapi?? Viwanja vyenyewe shida.
ReplyDeleteBaseball is growing. I believe one day it will be like other sports here in Tanzania. I play for kibasila and we won the national championships. It was one of the greatest things i have ever experienced
ReplyDelete