Home
Unlabelled
utii wa sheria bila shuruti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hili tangazo liko wapi?Inabidi afunguliwe mashitaka kwa makosa haya:
ReplyDelete(1) ubaguzi wa kidini; nchi yetu inasisitiza kuondoa ubaguzi wowote
(2) ubaguzi wa kijinsia
Kwa hiyo tunaomba mamlaka inayohusika kulishughulikia suala hili haraka iwezekanavyo; ni kiashiria kimojawapo cha uvunjifu wa amani. Nu hatari sana. Haba na haba hujaza kibaba.
Uhuru wa dini uko wapi ,uhuru wa mavazi ya mtu kujistiri uko wapi chini ya Tangazo hili. Avue HIJABU ili muone nini na kwa misingi gani na ni katika sheria gani.
ReplyDeleteHuu ni ubaguzi na kufata mkumbo wa mataifa ya magharibi kama vle ufaransa, waangaliaji wa picha twambieni wapi hapo tupajue..
ReplyDeleteAnonymous hapo hausemi kweli na sioni ubaguzi wa kidini, nikabu si vazi la kiislamu, vazi la kiislam kwa mafundisho ya quran na Hadith sahihi limeeleza wazi kuwa mwanamke vazi lake limsitiri mwili wake bila kuonesha maumbile yake isipokuwa uso, viganja vya mikono na nyayo bila kujali rangi au mtindo wa nguo, nikabu haijawahi kuwa vazi la kiislam zaidi ya kuwa la kiarabu , na uarabu na uislam ni vitu viwili tofauti. kiusalama na kimaadili inahatari kubwa na upo ushahidi mkubwa kuonyesha matumizi mabaya ya hiyo nikabu kiusalama na kijamii
ReplyDeletesheria namba ngapi hiyo? kwenye katiba ipi?
ReplyDeleteMwanamke avue Ninja ili uone nini?
ReplyDeleteKama ni Usalama imarisha Ulinzi kwa njia ambazo huingilii Itikadi za Kidini za Wateja wako na jamii!
Hilo tangazo lina maana gani?
ReplyDeleteBaada ya kuvuliwa Ninja ili iweje?
ReplyDeleteAu ndio utakuwa umefikia lengo lako?
Maana wengine 'hula na kushiba kwa ile kuona' tu!
mimi mwenyewe ni muislam na nimesoma shule ya dini, ila tuongee kweli si rasmi ktk uislam...Wanawake hatukuambiwa tufiche hadi macho yetu....
ReplyDeleteWanawake vinavyotakiwa kusitiriwa ni mwili yaani: Uvae km ni baibui mwisho ktk viganja vya mikono na chini hadi ktk fundo za miguu...Mtandio uvae..uufunge ufunike nywele uache paji la uso.
Tatizo walio wengi hupenda kukuza mambo... Na wadada wetu wa sasa huvaa hivyo si kwasababu ya kujisitiri bali wengine wanavaa ili kulinda ngozi yao ya uso isichomwe na jua iwe laini na nyeupe...Hasa wadada wa Kiarabu...
Utakuta mdada mchana kavaa ninja usiku utamkuta anatoka ktk mavazi ya uchi anaenda ktk starehe na wanaume wanamuona sasa hiyo ndio kafanya nini?
Mwanamke wa Kiislam jisitiri kama ulivyoamrishwa usikufuru sasa.. Angalia hata ktk Filamu za zamani za hadithi za mitume na visa mbali mbali..Huwaoni wakiwa wamevaa ninja hivyo !!!
Chakusikitisha zaidi sikuhizi wanavaa kufanyia uhalifu...
TUBADILIKE..
Pia tuzingatie sheria...Kuna sehemu na sehemu za kuvaa hiyo ninja...Ubalozini, Mahakamani,nk. si sehemu za kuvaa hivyo sababu kumekuwa na uhalifu mwingi sasa...
NAWAKILISHA
NI UBAGUZI WA DHAHIRI. HAKUNA CHENGINE. UNAANZA KUAMBIWA VUA NIKABU, BAADAYE UTAAMBIWA UVUE HIJABU, BAADAYE UTAAMBIWA UVUE GAUNI UBAKIE NA KIMINI, BAADAYE UTAAMBIWA UVUE NINI?
ReplyDeleteKWANI NIKABU INA TATIZO GANI? USALAMA SIKU HIZI UNAIMARISHWA KWA KUWA NA DNA, FINGERPRINTS, NA VIGANJA. DNA NA FINGERPRINTS NI UNIQUE KWA KIUMBE/MWANADAMU MMOJA.
TUBADILIKE, UBAGUZI UNAANZA TARATIBU TARATIBU. WAMASAI WANAVAA LUBEGA KILA PAHALA NA WANASEMWA NI UTAMADUNI WAO NA HAKUNA BUGHUDHA/USUMBUFU WOWOTE. NA WAMASAI KILA PAHALA WANALO JAMBIA KIUNONI NA MKUKI NI SEHEMU YA MILA YAO. NA HAKUNA TATIZO LOLOTE. WATU WENGINE UVAAJI WA NAMNA HIYO UNA WAKERA, LAKINI NCHI YETU INAJENGA UTAMADUNI WA KUVUMILIANA KWA KUWA KUNA WATU WA AINA MBALIMBALI MAKABILA MBALIMBALI NA DINI MBALIMBALI. HUWEZI KUMLAZIMISHA MTU KUFUATA KABILA LAKO AU DINI YAKO. NI HIYARI YA MTU KAMA KATIBA INAVYOSEMA.
KULE PAKISTANI KUNA MTU KWENYE MGAHAWA AKAANDIKA MGAHAWA HUU NI KWA AJILI YA WATU WA ULAYA TU. WATU WAKAJA JUU NA UKANYANG'NYWA LESENI MARA MOJA. MTU MWINGINE ANGESEMA KWAMBA KWA NINI ANYNG'ANYWE LESENI MTU SI ATAENDA KWENYE MGAHAWA MWINGINE. UHALISIA NI KWAMBA UBAGUZI UNAANZA TARATIBU.
KULE AFRIKA YA KUSINI WALE WABAGUZI WA RANGI WALIANZA TARATIBU. WAKAANZA HICHI CHOO NI WATU WA RANGI MAANA YAKE NI WATU WEUSI NA HICHI CHA WATU WEUPE. BAADAYE HILI BASI LA WATU WEUPUE NA HILI BASI LA WATU WA RANGI. BAADAYE WAKASEMA MTAA HUU WA WATU WEUPE NA MTAA HUU WA WATU WA RANGI (WEUSI).
HALI YA UBAGUZI IKAENDELEA HIVYO HIVYO HADI IKAWA NI UNYAMA WA KUTISHA.
NA HAPA NI HIVYO HIVYO, TUNAKEMEA KWA NGUVU ZOTE HILO TANGAZO NA ACHUKULIWE HATUA STAHIKI. HATUHITAJI AFRIKA YA KATI NYINGINE. TUSIWE WATETEZI WA UBAGUZI WA AINA YEYOTE ILE; LA SIVYO TUTATUMBUKIZA NCHI KWENYWE DIMBWI LA MACHAFUKO NA HAKUNA ATAKAYEWEZA KURUDISHA HIYO HALI.
ALIYETUUMBA ATUSAIDIE
Wengine hunyoa nyusi na huwa watisha kama bundi ndio maana huwa hawataki asiye husika kuona ndio maana avaa ninja. Na kama ni suala la kiusalama hapo na kama panahitajika kumjuwa mtu huyo kwa kuona kitambulisho chake,basi waweke mlinzi wa kike ,akamungalie na akiridhika sawa,end of story lakini kuweka bango kama hili yanaeleweka vyengine.
ReplyDeleteInaweza kuwa ni kosa kuweka bango hilo, na ikawa ni kosa kuingia kwenye halaiki umeficha uso, sasa jeee tumsaidieje mvaaji na mwenye duka. Tusikae kulumbana bila kutoa maoni ya nini kifanyike. Walio sema achukuliwe hatuwa nasema hawako sahihi, kwani uvaaji wa kufunika uso ni hatari dunia nzima, anaweza kuingia jambazi limevaa ninja likateka duka zima na wateja wooote mkatiwa mbaroni na likaondoka na kila kitu. Kila sehemu ya uhalifu huhusishwa na mavazi yasio rasmi.
ReplyDeletekuweka bango kama hilo sio tatizo bali inategemea hilo bango limewekwa wapi! kuna sehemu nyengine lazima uoneshe sura yako iliujulikanwe na camera za cctv zikuone, lakini kama unaenda sokoni na wewe ni mtu unaejiheshimu hutaki watu wakujue na kukukera kwa maongezi mengi unawea vaa nikabu, lakini kidini nikabu sio sharia. ijulikanwe hivyo!!!! tartibu za mavazi ya kiislamu zinajulikanwa na tartibu za tamaduni za mavazi ya baazi ya waarabu zinajulikanwa hivyo tusichanganye mambo katika dini, wala tusiipe mzigo dini kama ina sharia ngumu, laa! sharia za dini ni rahis sana bali TUJITAHINI KUSOMA ELIMU ILIYOKUWA NDIO SIO UBISHI TUU. thanks
ReplyDeletewhether uislam unafundisha au haufundishi, ku-inforce mavazi ni kinyume na sheria hasa katika taifa lisilo na dini ya utawala. Kila mtu ana haki ya kuvaa ngu apendayo. hiyo ninja ikivaliwa na pagani ni sahihi kabisa wana hana haja ya kujitetea. kama isilamu karuhusiwa basi ruhusa kwa wote. ndo maana ya democrasia.
ReplyDeletebiashara yako isiwe sababu ya kuingilia uhuru wa watu. kama ili biashara yako ifanikiwe lazima ubague basi serikali ichukue leseni yake.
suluhisho la jinai si kuingilia watu uhuru wao bali kuimarisha ulinzi.