Na Anna Nkinda – Maelezo

Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT)  umempongeza Mhe. Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kwa uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba linalotarajia kuanza leo Mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo Eva Mwingizi ilisema uteuzi wa Rais umezingatia umri, weledi, uzoefu na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii.

Mwingizi alisema uteuzi huo umeangalia asilimia 50 ya uwakilishi wa wajumbe 201 hii ikiwa ni wanawake 100 na wanaume 101 pia Bunge hilo linajumuisha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar.

Aidha katibu Mkuu huyo alilitakia heri Bunge hilo na kuwaomba wajumbe waliochaguliwa kutambua kuwa wamepewa dhamana kubwa ya kuzingatia maoni ya wananchi ya kutengeneza katiba ya Tanzania yenye kulinda, kutetea  na kusimamia maslahi ya Taifa kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...