HAYAWI hayawi, sasa yamekuwa! Ule uzinduzi wa albamu ya ‘Mtendwa Akitendewa’ kutoka bendi ya Extra Bongo kesho utafikia kilele ambapo watadondosha bonge la shoo katika ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem.
Akizungumzia maandalizi ya mwisho kuelekea shoo ya albamu hiyo katika hoteli maarufu ya Atriums iliyoko Afrika Sana, Sinza, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choky, alisema kila kitu kinaenda sawa na hivi sasa kilichobaki ni kudondosha mashambulizi siku ya kesho usiku.
Burudani hiyo itanoga zaidi kutokana na kusindikizwa na wakali wa Bongo Fleva kina Amin na Linah, Makhirikhiri wa Bongo, Bendi ya Mashujaa, TOT Band chini ya ‘Malkia wa Mipasho’ Khadija Kopa. Kiingilio kitakuwa ni sh. 6,000 tu.
HABARI/PICHA: ANDREW CARLOS, GPL
Titi Mwinyi katika pozi.
Banza Stone mmoja wa vivutio katika uzinduzi huo wa kesho.
Kiongozi Ally Choki Pongezi sana kwa kuonyesha moyo mzuri na nia nema kwa kuwepo Kunsini na nduguzo wa siku nyingi katika Gemu Miwnjuma Muumini na Ramadhani Masanja Banza Stone!
ReplyDeleteKweli Choki ni mfano wa kuigwa na Raisi mwema miongoni mwa Maraisi wa Bendi za Muziki Nchini!