Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla akielezea jinsi watakavyoweza kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwawezesha vijana kuleta maendeleo katika jamii, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi.
Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi akichangia wakati wa majadiliano ya awali jinsi ya kuendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla.
Mkurugenzi Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi akielezea kuhusu moja ya kituo cha vijana kinachojishughulisha na ufundi makanika kilichopo Ilonga Morogoro, kulia ni Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd Bw. Prashant Shukla wakati wa majadiliano ya awali ya kuendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Pro. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati alipokutana na Mkuu wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Ltd kujadili jinsi watakavyoweza kushirikiana kuanzisha program ya kuwaendeleza vijana kwa maendeleo ya jamii. Kushoto ni Bw. Prashant Shukla Mkuu ya kampuni hiyo na katikati ni Mkuu wa kitengo cha kozi fupi na ushauri chuo cha Mzumbe Pro. Shiv K. Tripathi ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Picha zote na Genofeva Matemu - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...