Wateja wa Vodacom wameendelea kukumbushwa kupata huduma katika maduka mapya yanayoendelea kufunguliwa maeneo mbalimbai karibu na makazi ili kuepuka gharama na usumbufu usio wa lazima wa kufuata huduma kwenye maduka yalyozoeleka yaliyopo mjini na yaliyo kwenye maeneo ya kibiashara. 
 Vodacom kwa sasa imekuwa ikifungua maduka sehemu mbalimbali ili kuwapunguzia gharama na muda wateja wake ikiwemo lilifunguliwa jana Tabata Magengeni jijini dar es salaam duka ambalo litatoa huduma kwa wakazi wa maeneo ya Tabata. 
 Mkuu wa idara ya Mauzo ya Rejareja wa kampuni hiyo, Upendo Richard amewataka wateja hao kutumia ipasavyo duka hilo na kuachana na kuepuka adha kusafiri kwenda mbali kutafuta huduma za Vodacom kwani duka hilo litakuwa likitoa huduma zote wanazo hitaji wateja wa kampuni hiyo. “Huduma katika maduka yetu yote bila kujali eneo lililopo yanatoa huduma zenye ubora sawa na za kiwango cha juu."lengo letu ni kuwasogezea wateja huduma karibu na walipo hivyo tunawaomba wayatumie kwa kujiamini na watapatapa suluhusho la mahitaji yao yote"aliongeza Upendo. 
 Kwa Upande wao wakazi wa Tabata Bwana, Saimon Edward Rugenga na Bi. Arafa Hamza ambao ni wateja wa kwanza kupata huduma katika duka hilo wamesema kusogezwa kwa huduma kwa wateja katika maeneo hayo ni jambo jema kwani sasa wateja wa matandao huo hawatopata tena tabu ya kusafiri kutoka Tabata kwenda maeneo mengine ya mji kufuata huduma hiyo. 
 “Eneo hili la tabata Magengeni ni eneo la makazi ya watu, tumezoea kuona maduka kma haya yakijengwa sehemu zenye maofisi au biashara, sasa kwa hatua hii ya kutuletea huduma hasa watu tulioko maeneo ya pembezoni mwa mji ni jambo jema ninaamini duka hili litatusaidia wakazi wengi na ninawasihi Vodacom wasiishie hapa Tabata waendelee katika maeneo mengine ya Mikoani,” alisema Bwana, Saimon Rugenga. 
 Nae Bi Arafa Hamza alisema “Kwa kipindi kirefu wateja wa Vodacom walioko tabata na maeneo ya karibu walilazimika kwenda Buguruni, Posta au Mlimani city ili kufuata huduma sasa jambo hili halitokuwepo tena, na yeye kama mfanyabiashara atakamilisha mahitaji yake yote ya kimawasiliano katika duka hilo, alisema.
Alihitimisha kuwa” Hatua hii ni yakupongezwa na watoa huduma za mawasiliano wengine waige mfano huu ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma hizi za mawasiliano kwa Watanzania.” 
Duka hilo ambalo ni la 77 kufunguliwa nchini litakuwa likitoa huduma mbalimbali zikiwemo ununuzi wa modem, kusajili laini, kuunganishwa na intaneti, kufanya manunuzi ya simu, huduma mbalimbali za M-Pesa pamoja na ushauri wa huduma za kimawasiliano.
 Muonekano wa duka jipya la Vodacom lililopo Tabata Magengeni.Duka hilo linatarajiwa kuwarahishia wateja kupata huduma kwa karibu na kuwapunguzia usumbufu na gharama za kufuata huduma umbali mrefu.
 Mkuu wa idara ya mauzo ya rejareja wa kampuni ya vodacom Upendo Richard akifungua mlango wa duka jipya la kampuni hiyo lililopo Tabata tayari kuanza rasmi kazi ya kutoa huduma. Kushoto ni meneja mauzo wa vodacom Tabata Michael Bigambo na kulia ni meneja wa duka hilo Simon Rugenge.
 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim (kulia) akimsikiliza  Saimon Rugenga ambae ni mteja wa pili kufika katika duka la Vodacom Tabata Magengeni mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Liganga alipongeza mkakati wa kampuni hiyo wa kufungua maduka kwenye maeneo ya makazi hatua itakayowapunguzia usumbufu na gharama wateja za kufuata huduma maeneo ya mijini na ya kibiashara. Katikati ni Meneja wa idara ya mauzo ya rejareja Elihuruma Ngowi. 
 Wafanyakazi wa Vodacom wakijumuika kutakiana heri na Saimon Liganga (wa tatu kushoto) na Arafa Hamza (wa nne kushoto)ambao ni wateja wawili wa kwanza kupata huduma kwenye duka jipya la kampuni hiyo lililopo Tabata Magengeni muda mfupi baada ya kufunguliwa rasmi jana. Vodacom inaendelea na mkakati wake wa kuwasogezea wateja huduma maeneo ya karibu na makazi yao.

 Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim akiokota kikaratasi cha mshindi wa zawadi ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom lililopo Tabata Magengeni. Droo hiyo ya kushtukiza ilihusisha wateja na wadau waliokuwepo wakati wa hafla ya uzinduzi.Mshindi alipatiwa moderm ya kisasa.
Mteja wa Vodacom Arafa Hamza akiagana kwa furaha na Mkuu wa Idara ya Mauzo ya Rejareja Upendo( kushoto) kwa  kubahatika kuwa mteja wa kwanza kupata huduma kwenye duka jipya lililopo Tabata Magengeni baada ya kuzinduliwa rasmi jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...