Ilikuwa patashika nguo chanika katika sherehe ya Harusi ya Alex Mwalwiba na Flora Japher  iliyofungwa katika kanisa la KKKT Mjini Lindi na baadaye mnuso wa nguvu  katika ukumbi wa Lindi Beach hotel.
  Bwana Harusi ni Fundi mkuu wa kampuni ya Uniglobex ya mjini lindi huku Bi Harusi akiwa mwajiriwa wa Jeshi la polisi Mkoani Lindi kitengo cha Usalama barabarani Sote kwa pamoja Tunawaombea Dua katika maisha yao Mapya ya Ndoa 
Picha na Abdulaziz Video Rec Ya Mjini Lindi
Wadau  Alex Mwalwiba na Flora Japher wakiwa na nyuso za furaha baada ya kumeremeta
 Alex Mwalwiba na Flora Japher katika taswira ya kumbukumbu Lindi Beach
Alex akiwa na wapambe
 Alex Mwalwiba na Flora Japher na wapambe wao
 Alex Mwalwiba na Flora Japher wakikata keki kwenye mnuso wao wa nguvu Lindi Beach hotel. Globu ya Jamii inawapongeza na kuwatakia maisha ya heri na ya furaha na yenye watoto kibao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mandhari ya Lindi mazuri, wadau wa Lindi wekezeni, miaka ijayo tusikie hata utalii Lindi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...