Wananchama wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu, Sayansi, Teknolojia, Habari na Utafiti nchini (RAAWU), Tawi la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wamekutana kwa semina ya siku mbili mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia pamoja na mambo mengine; masuala ya nafasi na wajibu wa kisheria wa vyama vya wafanyakazi katika kuleta tija na ufanisi sehemu za kazi. 
 Akifungua semina hiyo ya siku mbili kwa wanachama wa RAAWU tawi la HESLB, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Raslimali watu na Utawala Bi. Nuru Sovellah aliwaasa wanachama hao kutumia fursa ya Mafunzo yaliyokuwa yameandaliwa kutolewa katika semina hiyo ili kujifunza na kujikumbusha masuala ya kimsingi ya wajibu na Sheria wanapokuwa wanatimiza wajibu wao wa kazi. 
 Naye mwezeshaji wa Semina hiyo Bwana Sebastian Ndabani Inoshi a.k.a Seba aliwaasa wana-RAAWU kutumia semina hiyo kama njia ya kujiongezea wigo wa uelewa wa wajibu wa kisheria wa vyama vya wafanyakazi katika kuleta tija na ufanisi sehemu za kazi wakitambua kuwa ipo haja kubwa ya kuheshimu kazi kwa vile mfanyakazi anapopoteza kazi kwa uzembe hawezi kusaidiwa kwa kuwa hakutimiza wajibu wake kama alivyotakiwa. 
 Mada zingine zilizowasilishwa ni Wajibu wa Mwajiri na Mfanyakazi mahala pa kazi katika kuleta tija mahala pa kazi, umuhimu wa Mawasiliano bora mahala pa kazi, umuhimu wa utamaduni wa Taasisi katika kuleta tija na ufaniisi ndani ya taasisi na Dhana ya ufungaji wa mikataba ya hali bora katika kuboresha ustawi wa wafanyakazi. 
 Semina hiyo ya iliwajumuisha wanachama zaidi ya 70 wa Ofisi kuu Dar es Salaam na Ofisi za Zanzibar na Dodoma na ilifungwa kwa uongozi wa Bodi kuahdi kuendelea kutoa fursa ya Mafunzo ya aina hiyo kila mwaka kwa lengo la kuboresha ufanisi katika taasisi hiyo.

Mwezeshaji Bwana Sebastian Ndahani Inoshi a.k.a Seba (Kushoto) akiwasilisha mada. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Raslimali Watu na Utawala Bi. Nuru Sovellan na Kulia ni Kaimu Mwenyekiti RAAWU Tawi la HESLB Bi. Octavia Selemani.
 Sehemu ya wanachama wa RAAWU tawi la HESLB wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa katika semina hiyo.
Sehemu ya wanachama wa RAAWU tawi la HESLB wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa katika semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...