Mkuu wa mkoa wa iringa DK CHRISTIN ISHENGOMA amewataka wananchi mkoani  Iringa,kutokuwa na hofu katika kipindi hiki cha kuelekea kampeni za uchaguzi wa jimbo la kalenga.

Akizungumza leo  kwenye moja ya kituo cha redio mjini humo,Nuru FM ,kupitia kipindi cha sunrisepower, amesema kuwa tayari ameshakaa na kamati yake ya Ulinzi na Usalama akiwemo Kamanda wa Jeshi la Polisi,aidha ameongeza kuwa wamejiandaa kikamilifu katika ulinzi, hivyo wananchi wanapaswa kutokuwa na hofu.

Amesema kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi wa jimbo hilo wageni wengi watakuwa wanaingia hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na vishawishi vya makundi mabalimbali katika kipindi hiki cha uchaguzi.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kuwa yeye yupo katika vikao vya bunge maalum la katiba atakuwa anakuja kushiriki na wananchi katika mkoa wake katika shughuli mbalimbali zikiwemo za kampeni zinazoendelea.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kuhusu suala la posho kwa upande wake yupo tayari kupokea kiwango chochote atakachopewa ambacho kitakuwa kinatolewa katika kikao cha bunge maalum la katiba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...