Bango linalo onesha warsha ya kwanza ya Wadau wa Mfuko wa Misitu Tanzania
Mfuko
wa Misitu Tanzania ni Mfuko wa hifadhi ambao umeanzishwa kisheria kama
njia endelevu ya kuwezesha uhifadhi wa rasilimali za misitu hapa
nchini.Mfuko huu umeanzishwa kwa lengo la kukabiliana na changamoto za
usimamizi wa rasilimali za misitu hasa katika kuimarisha utekelezaji wa
Sera na Sheria ya Misitu.
Mfuko ilianza kazi rasmi Julai 2011.Mfuko wa
Misitu Tanzania ni wa Umma na unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini.Katika
utendaji wa kila siku,Bodi ya Wadhamini inasaidiwa na Sekretarieti.
Mfuko
wa Misitu Tanzania unafanya shughuli zake maeneo yote ya Tanzania Bara
ambapo hutoa ruzuku kwa wadau wote wanojihusisha na usimamizi wa
rasilimali za misitu na uboreshaji wa hali ya maisha ya wananchi waishio
pembezoni wa misitu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...