Wsanii 12 wakiwemo viongozi toka Shirikisho la muziki, Shirikisho la Filamu, Shirikisho la Sanaa za ufundi, Mtandao wa Wanamuziki Tanzania walifunga safari na kuvamia Dododma na kuwa na mfululizo wa mikutano na wabunge mbalimbali ili kuwashawishi waunge mkono vipengele viwili ambavyo wasanii wanavitaka katika Katiba
1. Kundi la wasanii kutambuliwa katika Katiba kama vile walivyotambuliwa Wakulima, wafugaji, wavuvi na wafugaji walivyotajwa
2. Milliki Bunifu kwa kiingereza Intellectual Property ambamo ndani yake kuna Hakimiliki itajwe rasmi katika Katiba hili litawezesha sheria mwafaka zitungwe katika kuendeleza sanaa na kulinda kazi za sanaa na kazi za ubunifu. Kundi hili limepokelewa vizuri sana na wabunge wote lililokutana nao
Mjumbe wa Bunge Maalumu la katiba Mhe Maria Sarungi akiwa na wawakilishi wa wasanii hao mjini Dodoma
Kikao kimoja kati ya vingi vya wasanii na wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba
Kikao kikiendelea..
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...