Mgeni Rasmi Daniel Kadinde akimkabidhi zawadi mwanafunzi Monalisa Sungwa aliyefanya vizuri katika masomo yake. Monalisa ni mmoja ya wanafunzi anayesomeshwa na Compassion.
Mgeni rasmi Daniel Kadinde akizungumza na watoto wahitaji katika ukumbi wa kanisa la Anglikana Ipogoro katika siku ya shukrani.
baadhi ya watoto wenye uhitaji wakifatilia kwa makini burudani iliyokuwa ikitolewa na kwaya ya watoto wenzao wa Ebeneza.
Kwaya ya watoto Ebeneza akitumbuiza katika siku ya kutoa shukrani kwa watoto wenye uhitaji iliyofanyika katika ukumbi wa Kanisa la Anglikana Ipogoro.
Mwanafunzi bora Monalisa Sungwa akisoma risala kwa niaba ya wanafunzi wenzake wanaosomeshwa na Compassion
========= ======= =========
WATOTO 287 WAFADHILIWA MASOMO NA COMPASSION IRINGA
Na Denis Mlowe,Iringa
JUMLA ya watoto wahitaji 287 wamefaidika na ufadhili wa masomo ya elimu ya shule ya msingi na sekondari unaotolewa na Kituo cha Huduma ya Mtoto cha Anglikana Ipogoro kwa ufadhili wa shirika la Compassion.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kituo hicho Kaini Mwakisyala wakati akiongea na mwandishi wa habari hizi wakati wa siku ya Shukrani kwa Watoto wahitaji uliofanyika katika kanisa la Anglikana tawi la Ipogoro mwanzoni mwa wiki.
Mwakasyala alisema kuwa watoto walionufaika na ufadhili huo ni kutoka mikoa sehemu za Ilula, Ipogoro na maeneo jirani ya wilaya ya Kilolo huku wengi wao wakiwa ni watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kwani moja ya malengo ya Taasisi hiyo ni kuwasaidia watoto wenye mahitaji hasa wa kike ili waweze kupata elimu sawa na watoto wengine walio na wazazi.
“Watoto hawa wako katika shule za Bweni hii ni kuwafanya waweze kupata huduma zote muhimu ambazo ni chakula, malazi na muda wa kujisomea kwani watoto wengi wa kike wakisoma shule za kutwa wanatumia muda mwingi kufanya kazi za nyumbani na hivyo kukosa muda wa kujisomea na kucheza michezo mbalimbali” alisema Mwakasyala.
Alisema kuna umuhimu wa watoto wa wa jinsia zote kupa elimu itakayomsaidia katika maisha yake ya kila siku na shirika hilo linamsomesha mtoto hadi anapofikia elimu ya chuo na baada ya hapo atakuwa na uwezo wa kujiendeshea maisha yake.
Mwakasyala alisema watoto wa kituo hicho licha ya elimu ya kawaida wanapa elimu ya ufundi wa kushona nguo, kufyatua matofali na ufundi mwingine unaoweza kuwakomboa mara wamalizapo elimu zao na elimu hiyo hutolewa kutokana na vipaji walivyonavyo.
Aidha aliwataka wazazi kuwapa ushirikiano katika kuwaleta watoto waweze kupata elimu stahiki kwa kugharamiwa kila kitu na shirika hilo zikiwemo ada, sare za shule na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
Mwakasyala alibainisha changamoto wanazokumbana nazo mojawapo ni wazazi wengi kushindwa kuwaleta watoto wao kwa misingi ya dini wakidhani kwamba wakiwapeleka katika kituo hicho watabadilishwa dini walizozaliwa nazo kutokana na chuo kumilikiwa na kanisa la Anglikana.
Kwa upande wao watoto wa kituo hicho wakiwakilishwa na Monalisa Sungwa wa kituo hicho alitoa shukrani kwa uongozi wa kituo hicho kwa kusimamia huduma zote kwa watoto hao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuwakomboa katika kupata elimu iliyobora.
Sungwa aliitaka jamii kuwashirikisha katika maswala ya kijamii kwa ngazi ya kiwilaya katika kutoa maoni kutokana na mtoto kuwa na haki katika kutoa maoni kwa jamii inayomzunguka.
“ Tumekuwa hatupewi fursa nyingi za kushiriki katika mafunzo na matamasha pamoja na shughuli zingine za kijamii hakika hii inasababisha ushiriki mdogo katika masuala ya kijamii naomba sana tushirikishwe katika kutoa maoni” alisema Sungwa
Aidha alisema wanakumbana na changamoto ya wazazi kutokuwa na ushirikiano na kituo hasa pale wanapohitajika kushirikiana katika kuwafatilia watoto maswala ya shuleni na tabia za watoto kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...