
Washtakiwa hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na aliyekuwa Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga (55) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka dhidi ya washtakiwa, mahakama imeona wana hatia kwa makosa yote matano.
Alisema hati ya mashitaka inaonyesha mshtakiwa wa kwanza anakabiliwa na mashitaka watatu na upande wa mashitaka umethibitisha kweli alitenda makosa hayo na mahakama inamhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kila kosa au kulipa faini ya Sh. Milioni 3 kwa kila kosa.
Kwa upande wa mshtakiwa wa pili, hakimu alisema hakuna ubishi bila kuacha shaka mshtakiwa, alitenda makosa hayo na kwamba atalipa faini ya Sh. Milioni 3 kila kosa au kulipa fani ya Sh. Milioni 3 kila kosa. Hata hivyo, walilipa faini hiyo na kuachiwa huru.
Katika kesi ya msingi, washtakiwa walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matano ya matumizi mabaya ya ofisi katika utoaji kibali cha ujenzi wa jengo la ghorofa 15 kiwanja namba 45 mtaa wa Chimara.
Ilidaiwa kuwa Kimweri alikuwa na wadhifa huo TBA kuanzia mwaka 2002 hadi 2010 na Maliyaga aliajiriwa mwaka 2002 akiwa msanifu mkuu.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai alidai kiwanja hicho kilikuwa kinamilikiwa na TBA, ambako hadi mwaka 2006 kilikuwa hakijaendelezwa.
Aidha TBA, kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma iliwaalika wanaotaka kuwekeza kuwasilisha andiko la awali kwa ajili ya uendelezaji.
Wote wamelipa faini na kuachiwa huru
Wote wamelipa faini na kuachiwa huru
peanut fine!
ReplyDeleteukiona hivyo kila mtu kashachukua chake hapo, ulaji ulaji tuuuu bongoooooooo
ReplyDeleteKwa hivyo jengo litavunjwa?
ReplyDeleteama kilicho onekana ni hatari kuwepo jirani na Ikulu baada ya kuhukumiwa kimeyeyuka?
Kama ikulu wanaogopa ilo jengo kwa madai ya kuwa refu sana walinunue wao liwe mali ikulu ,litumiwe ama na wafanyakazi wa ikulu au matumizi mengine ya kiserikali yasiyo hatarishi kwa usalama wa viongozi wa nchi.
ReplyDeleteWekeni maoni yote mlio tumiwa bila kubagua.,kwani kufanya tofauti ni kukiuka uhuru wa habari,uhuru wa kujieleza na haki ya mtoa maoni kwenye chombo hiki kama kilivyo na matumizi yake.
ReplyDeleteSuluhisho kwa jengo hilo:
ReplyDelete1.Tunahitaji Usalama kwa Viongozi na nchi.
2.Hapo hapo Uchumi na Miundo Mbinu ya majengo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.
Hamuoni Serikali ina Kopa ili kujenga?
Suluhisho Jengo liachwe liwe mali ya Serikali litumike kwa kufugia kuku wa mayai na nyama na mbuzi kuanzia Ghorofa ya 7 hadi ya 18 !
Ghorofa za chini 1 hadi 6 Ruksa kwa matumizi ya watu!
Jengo chini Ghorofa ya 6 hadi chini magtumizi ya watu na juu liwe Gereza la Wauza Unga wanapo shikwa China kuanzia Ghorofa ya 7 hadi ya 18 !
ReplyDelete