Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu akiongea na watoto
wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijiini Dar es Salaam,
wakati alipofika kituoni hapo kutoa
msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na mashine ya kusagia juisi,
alipoguswa kama mzazi na
maisha ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania, Mizinga Melu akifurahia jambo na
baadhi ya watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Msimbazi centre jijini Dar
es Salaam,alipowatembelea na kuwakabidhi msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo
vyakula.
Baadhi
ya watoto yatima wanaolelewa katika
kituo cha Msimbazi Centre jijini Dar es Salaam wakipokea zawadi za biskuti toka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya biashara ya NBC Tanzania,Bi. Mizinga Melu,walipotembelea
na mkurugenzi huyo kama mzazi na kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo
vyakula pamoja na mashine ya kusagia juisi.
Mkurugenzi Mtendeji wa benki ya Biashara
ya NBC Tanzania,Bi. Mizinga Melu(kulia)akimuongelesha jambo mmoja wa watoto
wanaolelewa katika kituo cha Yatima cha Msimbazi Centre jijini Dar es
Salaam,alipotembelea kituo hicho kama mzazi aliyeguswa na maisha ya watoto hao
na kutoa msaada wa vitu mbalimbali,Kushoto ni
Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda
Songoro.
Mkuu wa kituo cha Kulelea watoto yatima
cha Msimbazi Centre Sister. Ehienne(kushoto),akipokea moja ya msaada wa katoni
ya pambazi kwaajili ya matumizi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho toka
kwa Mkurugenzi Mtendeji wa Benki ya
Biashara ya NBC Tanzania,Bi.Mizinga Melu(katikati)
Mkurugenzi huyo alikabidhi vitu mbalimbali kama vile mchele ,mafuta na mashine
ya kusagia juisi baada ya kuguswa kama mzazi na maisha ya watoto hao
wanaolelewa katika kituo hicho,kulia ni
Katibu Mhitasi wa benki hiyo Jolanda
Songoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...