Waziri wa Afya
na ustawi wa Jamii katika picha ya Pamoja na mgeni rasmi Rais wa Idnia Dkt. .APJ Abdul Kalam baada ya kufungua kongamano linalojadili matokeo ya
tafiti mbalimbali zinazohusu magonjwa ya saratani,hatua za kujikinga na
magonjwa ya saratani,tiba za magonjwa ya saratani.mkutano huu uluhudhuriwa na
washiriki mbalimbali kutoka bara la Afrika na Asia.Kulia kwa waziri wa Afya ni
waziri wa Afya wa Zimbabwe Mhe David Parirenyatwa
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii akifanya mazungumzo na mwenyekiti wa hospitali za appollo Dr.Pratap Reddy(mwenye tai ya bluu).mhe.waziri alikuwa akihudhuria kongamano la ugonjwa wa Saratani nchini India.mazungumzo haya yalilenga kuboresha utoaji wa huduma za Afya nchini Tanzania hususan Ugonjwa saratani.
Washiriki kutoka mataifa mbalimbali katika
kongamano la saratani nchini India,wakimsikiliza waziri wa Afya na ustawi Jamii
Dkt.Seif Rashid alipohutubia kongamano Hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...