Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamataifa katika Ofisi za Idara ya Habari (Maelezo). Wakati wa Mkutano huo Mhe. Membe alizungumzia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutetea suala la Uraia wa Nchi mbili kwa Watanzania waishio ughaibuni kupitia Bunge Maalum la Katiba, Kuchaguliwa tena kwa Tanzania kwenye Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Nafasi ya Tanzania katika Ulinzi wa Amani duniani na kuendelea kudumisha Uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Rwanda. Wengine katika ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Rajabu Gamaha (wa pili kutoka kushoto), Balozi Simba Yahya (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati na Bw. Assah Mwambene Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).
Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kushoto) akisikiliza kwa makini mkutano kati ya Mhe. Waziri Membe na Waandishi wa Habari (hawapo pichani). Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya  Habari, Bi Zamaradi Kawawa na  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.
Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati yao na Mhe. Membe.
Mhe. Waziri Membe akisikiliza maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipozungumza nao. Mkurugenzi wa Afrika, Balozi Vincent Kibwana (wa pili kulia) na Bibi Rosemary Jairo (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakati wa mkutano huo.Picha na Reginald Kisaka 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...