Msanii aliyetamba enzi hizo kwa umahili wake wa kucheza na nyoka Salma Moshi akisalimiana na kumkabidhi picha za baadhi ya kazi ya sanaa hiyo aliyofanya enzi hizo kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula alipokwenda kujitambulisha rasmi kwenye Ubalozini wa Tanzania uliopo Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014.
Msanii wa siku nyingi na mahili wa kucheza na nyoka Bi. Salma Moshi akiongea na Mhe. Balozi Libetara Mulamula alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tamzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula akimsikiliza msanii wa siku nyingi, Bi Salma Moshi (hayupo pichani) alipotembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC siku ya Jumanne Feb 18, 2014.
 Afisa wa Ubalozi,Bw. Mgendi Nzowa akiwa kwenye mkutano huo.
 Afisa wa Ubalozi,Bw. Suleiman Saleh akijumuika pamoja na Balozi kwenye mkutano huo.

Wito huo umetolewa na msanii wa siku nyingi wa kucheza na nyoka Mama Salima Moshi alipokwenda kumuona, Balozi wa Tanzania nchini Marekani,Mh. Liberata Mulamula.

Mama Salima alisema Balozi zina nafasi nzuri za kuutangaza utamaduni wetu kwani wapo karibu na nchi husika na hivyo kuviwezesha vikundi kuja kufanya maonyesho mbali mbali katika nchi husika.

Pia aliliomba BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA) kuandaa kitabu kitakachojumuisha wasanii mbalimbali na anwani zao,vitabu hivyo vipelekwe kwenye balozi zetu ili watu mbalimbali wanaokuja waweze kuvisoma na hatimaye kuwaalika wasanii watakaoweza kuutangaza utamaduni wetu na wasanii kujipatia kipato na pia kujifunza. 

 mama Salima alisema MAPROMOTA wengi baada ya kupata wamekuwa wanawatelekeza wasanii na pato kubwa linaenda kwao bila kunufaisha msanii,na hata wale wanaobahatika kuja kupiga nje wamekuwa wanaishia kuwapigia watanzania,ifike wakati wakija huku waweze kutumbuiza na wenyeji wa huku.

Alitoa mfano kama Jay Z aende Tanzania halafu awapigie Wamarekani wenzake tu,pia swala la kukopi kazi za sanaa linarudusha nyuma maendeleo ya wasanii na aliomba SERIKALI kutoa adhabu kali kwa watakao bainika na kusimamia swala la hakimiliki.

Kwani imefika wakati sasa wasanii kuwa na WANASHERIA hii itasaidia kulinda haki zao,Mama salima alimshuru sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa karibu na wasaniina wakati wote hata hivi karibuni aliwaalika kwenye chakula hivyo naomba wasanii tuitumie nafasi hiyo.

 Alisema kuhusu tunzo ziwe zinatolewa kwa wasanii wa sanaa za maonyesho na wakati umefika kutoa kibali kwa waandaaji wengine si vibaya zikawa zaidi ya moja,pia aliomba kusaidia kujenga maktaba kwenye eneo la viwanja vya wasanii MKURANGA na kumpongeza mwenyekiti wa wasanii bw TWALIBU 

 MH BALOZI alimshukuru sana msanii huyo na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuwakilisha nchi na kuwa msanii atakayekuwa mfano kwa wengine alisema kuhusu Hakimiliki SERIKALI imejizatiti kikamilifu kuhakikisha haki za msanii zinalindwa alisema ni vyema wasanii wakajua haki zao hii itawasaidia sana aliongolea MAPROMOTA ni vyema kuangalia maslahi ya wasaniikwanza MH Balozi alisifu sana kazi zinazofanywa na wasanii mbalimbali nchinina kuitangaza NCHI yetu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...