Hotuba ya Mwalimu Nyerere hoteli ya 
Kilimanjaro jijini Dar es salaam June 14, 1994

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Safi sana. Na kipindi hiki ni muafaka kusikiliza busara za mpendwa mzee wetu Mwalimu Nyerere. Kweli alikuwa zawadi kubwa kwetu. He was a truly gifted speaker, ambae hakuchukua hata personal notes za maswali aliyokuwa akiulizwa zaidi ya kusikiliza na kuweza kujibu hoja zote. Baada ya kuondoka mwalimu sasa nimeamini usemi you never appreciate what you have until is gone.. I appreciate guidance ya Mwalimu now and miss his guidance to our country more now than ever..At least we have his speeches.. huu ndio wosia kwetu.

    ReplyDelete
  2. ANAONGOZA AKIWA KABURINI.

    ReplyDelete
  3. Hivi inamaanisha Mh Jaji Warioba hakuwahi kuisikiliza hii speech...?

    Where does he (Jaji Warioba) want to take us with the so called serikali tatu?

    Jaji Warioba kuna mengi anayotakiwa kutujibu......

    ReplyDelete
  4. Tarehe ya leo ni 20 Feb 2014

    ReplyDelete
  5. Ankal Michuzi,
    Tafadhali sana tuwekee pia Hotuba ya Baba wa Taifa Mwalimu J.K. Nyerere aliyoitoa Bungeni Dodoma tarehe 1 Februari, 1984 alipokuwa akielezea sababu iliyomfanya ajiuzulu aliyekuwa Makamu wa Rais wa wakati huo Aboud Jumbe.
    Baba wa Taifa alielezea kiundani sana kuhusu Muungano wetu wa Tanzania. Sasa katika kipindi hiki cha Kutengeneza Katiba Mpya ni kipindi muafaka na muhimu sana kuisikiliza tena hotuba hiyo.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete

  6. Tunamuombea huko aliko

    Ni wazi asingependa watu fulani si tu kwamba wasigombee uraisi 2015 bali pia hata fomu wairuhusiwe kuchukuwa kwani wamekwisha kutuonyesha kuwa wana uchu wa kukimbilia Ikulu.

    Na hasa wanataka kwenda ikulu kwa gharama yeyote ile...

    Uchaguzi 2015 bila watu hawa INAWEZEKANA

    ReplyDelete
  7. Mwalimu si alimkataza mmoja wa wagombea 1995? Mbona huyu mgombea ndio anataka kuwa mgombea tena 2015?

    ReplyDelete


  8. LOKASA YA MOBALI NA NGAI

    TANZANIANS ARE NOT FOOLS (CCM ALSO ARE NOT FOOLS LIKE YOU THINK.

    ReplyDelete

  9. Kumbe Mwalimu ulikuwa unazuia ndoto za watu zisitimie. Sasa ona haupo wenye ndoto zao wanamwaga mipesa wazi wazi na kusema hiyo ni mikakati yao ya kwenda Ikulu ... kwani wanajua wadanganyika ni wadanganyika tu ... aliyekuwa anawafumbua NA KUWALINDA SASA HAYUPO.

    ReplyDelete
  10. msimlaumu jaji warioba walaumuni wanzanzibari ambao wamechoka kunyonywa na walaumuni watanganyika ambao kwa miaka mingi nchi yao ilimezwa dunia imebadilika sio wakati wakuchangiwa akili tunataka muungano wa haki kwa pande zote mbili tuwe na muungano imara utuvushe miaka.50 ijayo

    ReplyDelete
  11. Baba wa taifa aliyasema na kuyaamini mambo mengi, mbona hatuongelei azimio la arusha na uuzaji wa mali za taifa kwa bei ya bure? Dunia imebadilika na inawezekana hata yeye angekuwepo angeona ni bora serikali tatu kuliko kero hizi kwa miaka 50, wanaopinga serikali tatu hawajibu namna ya kuondoa kero ambazo zimeshindikana baada ya miaka yote hiyo ya muungano1!!

    ReplyDelete
  12. Asante kwa kumbukumbu hii. Hii ni mojawapo ya hotuba ambayo ingekuwa ni lazima kwa hawa wajumbe watakiwe kuisikiliza. Miaka karibu 50 ya muungano na bado kungali na matundu ya tofauti zetu eti kati ya "watanganyika" na "wazanzibari". Bila elimu ujinga na umasikini haviondoki. Sasa ni muda wa kujenga serikali moja na siyo tatu (3). Serikali tatu ni leseni ya kuvunja muungano.

    ReplyDelete
  13. Anonymous namba 2.
    Sidhani kama unajua kuwa ulichokisema ni kama dharau kwa Watanzania kuwa wanaongozwa na mfu kaburini.

    ReplyDelete
  14. KWELI NAMBA 2 KAWADHARAU WATANGANYIKA, TUNAONGOZWA NA MFU? HAIKUBALIKI KABISA? YEYE MUDA ULISHAPITA NA HUKO ALIKO ANAULIZWA ALIYOYATENDA.

    SASA TUJE WEWE NA MIMI, KABLA UMAUTI HAUJATUFIKA. TUMEIFANYIA NINI TANGANYIKA? MESHIMIWA RAIS KIKWETE ALIVYOWAHUTUBIA WAFANYAKAZI MIAKA YA NYUMA ALISEMA UNATAKIWA UWE KAMA MBAIWAI, YANI LA KUAMBIWA UCHANGANYE NA AKILI YAKO ILI UWEZE KUWA NA MAAMUZI BORA...

    ReplyDelete
  15. Mfano mzuri wa kuvunja muungano upo pale Sudan.Sudan(Juba) waliomba kujitenga kutoka Sudan kuu(Khartoum).Wakajitenga,mmeona kinachotokea sasa Sudan Kusini?Wanapigana wao kwa wao.Lisemwalo lipo.Muungano udumu!

    David V

    ReplyDelete
  16. SUDANI KUSINI HAIKUWA NCHI KABLA; ZANZIBAR NI NCHI NA TANGANYIKA NI NCHI; KAMA UNAVYOOMA UK AMBAPO SCOTLAND, WALES, NA ENGLAND NI NCHI ZINAUNDA UK. KWA HIYO CHA MSINGI KUWEKA MAMBO SAWA KATI YA TANGANYIKA NA ZANZIBAR.

    YANI NCHI YA ZANZIBAR IWEPO NA NCHI YA TANGANYIKA IWEPO. NCHI HIZI MBILI ZITAKUBALIANA MAMBO YA KUSHIRIKIANA.

    VURUGU/VITA ZA WENYEWE KWA WENYEWE ZIKO SEHEMU NYINGI; AFRIKA YA KATI, MALI, UKRAIN, UHISPANIA, DRC, SOMALIA, N.K.

    LILILO LA MUHIMU NI KUWA NA SIASA SAFI NA UTAWALA BORA. SUDANI KUSINI WATU WAKE ASILIMIA KUBWA HAWANA ELIMU, NIKISEMA ELIMU SIMAANISHI KUJUA KUSOMA GAZETI LA UDAKU NA KUANDIKA BARUA HAPANA. ELIMU KWA MAANA KUJUA KUTENDA KITU FULANI NA KUKITUMIA ILI KUPATA MLO MWEMA, NYUMBA BORA, MAJI SAFI, N.K.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...