KAMPUNI mpya ya usambazaji wa filamu Bongo ya Yuneda Entertainment imeingia katika biashara ya usambazaji baada ya kilio cha wasanii kukosa sehemu za kuuza filamu zao au kusambaziwa
Kampuni hiyo inayojali ubora kwa kazi za sinema imeingia nchini kuanza kwa kusambaza filamu ya Why Linah?
Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii nyota katika tasnia ya filamu Bongo kama Hemed Suleiman ‘Phd’, Rose Ndauka, Charles Magali ‘Mzee Magali’, pamoja na wasanii wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu Swahilihood, filamu hiyo inaingia leo jumatatu.
Wasanii wamefurahia sana ujio wa kampuni hiyo kwani wanaamini kuwa wengi wataweza kusambaziwa kazi zao kwani moja ya sifa hiyo ni ya kizalendo inayojali maslahi ya wasanii, na inaongozwa na wazalendo wanaojua hali halisi ya soko la filamu nchi Tanzania.
Hivyo kwa kuzingatia umakini na ubora wa filamu Yuneda Entertainment wanakuletea filamu yenye viwango vya kimataifa ya Why Linah?.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...