Daktari Bingwa wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu Dr. Othman W. Kiloloma kutoka hospitali ya Muhimbili amesema kuwa timu ya madaktari saba imewasili kutoka Muhimbili ikiwa na daktari bingwa 1 wa usingizi wakiwa na vifaa vyote muhimu ili kuungana na madaktari Bingwa wa upasuaji Bugando kwaajili ya kuweka kambi ya tiba mkoani Mwanza.
|
Dr. Othman W. Kiloloma ameongeza kuwa dhana ya kuweka kambi Mwanza imekuja ikiwa ni hatua ya kujaribu kupunguza vifo na usumbufu unaowakumba watu wenye maradhi hayo pindi wanapohitaji tiba ambapo wengi wameshindwa kupata huduma mapema kutokana na kushindwa kuzimudu gharama kwa magonjwa hayo ambayo kila kukicha idadi ya watu wenye matatizo ya Ubongo na Mishipa ya fahamu inaongezeka. Ameishukuru sana African Barrick Gold kwa kudhamini mpango huo.
|
Kama upasuaji utahitaji kufanyika masaa 24 tuko tayari kwa hilo, nia ni kuwahudumia wale wote watakao jiandikisha kuwa wanamatatizo na wanahitaji tiba.
|
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA |
Kazi nzuri Bugando, lakini haya mambo ya vitanda kulaliwa na zaidi ya mgonjwa mmoja kwenye baadhi ya wodi za watoto za hospitali za rufaa yatafutiwe ufumbuzi na uongozi wa hospitali hizi kwa kuongeza vitanda katika mikakati ya kuendeleza hospitali.
ReplyDelete