Suala la uraia pacha sio geni duniani. Uraia pacha ulianza zamani kwa baadhi ya nchi lakini kwa nchi yetu ya Tanzania ni suala jipya kabisa lakini katika historia ya dunia uraia pacha sio jambo geni.
Hivyo cha kusema labda ni kuwa Watanzania tunaoishi Tanzania
tusiwashangae Watanzania wa ughaibuni wanaolipendekeza suala hili ili kuilinda haki yao ya msingi ya kuzaliwa Tanzania na kutuomba Watanzania wote tuliunge mkono.
tusiwashangae Watanzania wa ughaibuni wanaolipendekeza suala hili ili kuilinda haki yao ya msingi ya kuzaliwa Tanzania na kutuomba Watanzania wote tuliunge mkono.
Sisi tunaoishi Tanzania ni Watanzania na wao ni Watanzania vile vile. Suala la “Mimi ni Mtanzania” ni suala ambalo linatoka moyoni mwa mtu jinsi anavyojisikia yeye ana utaifa gani. Kama ni Mtanzania hata kama anaishi Kenya au China bado ni Mtanzania mwenzako.
Wasiwasi uliopo Tanzania wa kuruhusu uraia pacha unaeleweka kabisa na nchi zilizo na uzoefu na suala hili. Kihistoria suala la uraia pacha lilianza kale tangu enzi za Wagiriki na Warumi.
Na kabla ya hapo watu walikuwa wakisafiri na kubadilisha makazi yao. Wakati ule Mataifa makubwa yalikuwa chini ya Wagiriki na Warumi. Tutakumbuka hata Socrates alipoulizwa alikuwa raia wa nchi gani alijibu na kusema yeye ni raia wa ulimwengu, wakati alitakiwa kujibu kuwa alikuwa raia wa Athens au wa Corinthian.
Kihistoria, kwa Socrates uraia wake wa dunia ulimsaidia sana kuwa karibu na watu wengine kutoka mataifa mengine na vile vile ulimsaidia katika kueneza filosofia za Wagiriki ulimwenguni. Hata Watanzania waliopo sehemu nyingine duniani ndio chachu ya kuendeleza utamaduni wa Mtanzania na uzalendo wa Kitanzania duniani na sehemu yeyote walipo.

Kwa mfano kama ilivyo diplomasia ya Tanzania inayoangalia zaidi masuala ya uchumi, diplomasia ya uraia pacha inaweza kabisa kutufanya tukawa taifa lenye nguvu zaidi duniani. Kumbuka sisi Watanzania tunapendwa sana na tunatambulika kwenye kila kona ya dunia kwa kupenda amani, mshikamano na umoja. Hivyo tunaweza kabisa kuitumia diplomasia ya uraia pacha kuijenga Tanzania yenye nguvu na yenye sauti kubwa ndani ya Afrika na dunia kwa ujumla.
Uraia wa pacha unaweza ukaongeza ufanisi katika shughuli za serikali kwa kuleta suluhisho kwenye changamoto nyingi zinazolikabili taifa. Kwa mfano, uraia pacha unaweza kutufundisha namna ya nchi nyingine zinavyofanya kazi kwa kuwa raia wetu watakuwa wakifanya kazi katika nchi hizo na wanaweza wakaleta mazuri ya ughaibuni na kuyaunganisha na mazuri ya Tanzania katika kupata taasisi na vyombo vya umma vinavyofanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.
Umoja wa Watanzania hautapotea kwa kuruhusiwa kuwepo kwa uraia wa nchi mbili kwa sababu Watanzania wote tunaunganishwa na historia yetu iliyoanza tangu enzi za mababu zetu.
Na tukumbuke kuwa si kila raia yeyote wa nje atapewa Utanzania. Uraia wa Tanzania atapewa mtu ambaye anakubalika na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtu ambaye amekubalika kuwa Mtanzania. Na uraia wa Tanzania hautagawiwa kama njugu. Tunapendekeza viwepo vigezo muhimu vya kumpatia mtu uraia wa Tanzania.
Hivyo sio kweli kwamba Tanzania itajaa wageni tu yaani watu wasio na asili ya Kitanzania. Kuna namna nyingi za kulitekeleza suala hili kwa sheria zitakazotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nadhani Watanzania walio wengi watukubaliana na pendekezo hili. Uraia pacha kwa watu wenye asili ya Tanzania ndio.
Lakini kwa watu wasiokuwa na asili ya Tanzania kupata uraia wa Tanzania iwe ngumu kidogo kwao ili uraia wa Tanzania usigawiwe kama njugu na husiwe rahisi kuupata bila kufuatisha sheria zilizowekwa na nchi. Tunadhani kila nchi yenye uraia pacha inafanya hivi.
Tunazidi kuliomba Bunge Maalumu la Katiba lizingatie maoni yetu na liruhusu uraia pacha lakini kwa sheria zitakazowekwa kulinda usalama wa Taifa la Tanzania. Hili ni suala linalowezekana.
Tunaomba Wabunge wote wampe kila ushirikiano Mheshimiwa Kadari Singo anayewakilisha Watanzania wa Diaspora kwenye Bunge Maalumu la Katiba atakapotoa mapendekezo yake kuhusu suala hili.
Imeandaliwa na Deogratius Mhella, Katibu wa Vikao vya Jumuiya za Watanzania Marekani na DICOTA katika jitihada za Watanzania waishio ughaibuni kuelimisha umma kuhusu Watanzania wa ughaibuni na kuhusiana na suala zima la uraia pacha.
Kenya,Uganda,Rwanda hata na Burundi wote wanaruhusu Uraia pacha.Hizo inchi zilizo na urai pacha hazijawahi kuingia matatizoni eti kwa sababu ya urai pacha.
ReplyDeleteDual citizenship is the thing of future.
ReplyDeleteWana EAC(Uganda,Rwanda,Kenya,Burundi) wameisha tuacha katika hili.Thanks Lord halikuwa suala la kijumuia. Amasivyo tungeanza kulalamika kuwa tumetengwa.
ReplyDeleteSisi wa TZ ni wepesi kusaini mikataba isiyo na Tija kwa wananchi.Mengine tunajivuta na hatujiamini.
ReplyDeleteBila uraia pacha, watanzania tutazidi kuwa na nawazo mgando kama huna hoja ni busara kukaa kimya. Fikiria kama ni ndugu yako yuko nje j miaka mingi utapinga suala hilo? au kwa sababu haikuhusu? Na wengi wanaopinga hawana hata rafiki wala ndugu nje, kwa hiyo halikuhusu lakini kama Mtanzania linakuhusu. Nimetembea nchi nyingi na kukutana na Watanzania hawa Upendo walionao kwa Tanzania ni mkumbwa mno tofauti na sisi tuliopo nyumbani. Kwa hiyo ni wajibu wetu kuwalinda na kuwathamini kama ndugu zetu. Mlinzi wa Tanzania ni sisi Watanzania Wenyewe hata kama unamakarasi ya uraia nchi nane badi wewe ni Mtanzania cha muhinu kuweka mazingira ya kumbana pindi anapohirajika nyumbani.kwa mfano kimichezo.
ReplyDeleteKweli raia wa Tanzania haijalishi anaishi nchi gani ni mtanzania.
ReplyDeleteMdau wa nne usiseme hatujiamini, watanzania tunajiamini sana labda useme hivyo kwa nafsi yako mwenyewe lkn usijumuishe watz wote.Tumethubutu,tumeweza na tunazidi kusonga mbele.
ReplyDeleteWatanzania wanao jaribu kulitilia fitina jambo la uraia pacha si kwamba hawaoni umuhimu wake ! wanajua kabisa dunia ya sasa ina mabadiliko lakini wanaona kijicho kwanini? wachache walio nje wawe na uteule fulani na wengine wasiwe,hapa ndipo panapojaa nongwa
ReplyDeleteSi muhamie huko, kwani ni lazima muendelee kuwa watanzania ikiwa mna hamu na umarekani, uingereza ama hata huo uchina?
ReplyDeleteSidhan kama kuna binadamu amelazimishwa kwenda kuishi nje, ila ameenda kwa maslahi yake
In Tanzania citizen registration database,there is no room for those who are grown up,only remain space for the new born children .Sori guys.
ReplyDeletenina uraia wa australia lakini bado najihisi na kujivunia tanzania tanzania ni nchi yangu na naipenda kwa roho moja
ReplyDelete