Habari na picha na John Nditi, Morogoro
Kuanzia aljafiri leo, madereva wa daladala wanaoendesha magari yao ya abiria katika njiaa mbalimbali za Manispaa ya Morogoro waligoma kutoka huduma hiyo kwa muda wa saa 10 wakishinikisha kutendewa haki ya Kikosi cha Usalama Barabarani. 
 Madereva hao kwa umoja wao Machi 18, mwaka huu walipomaliza kazi yao usiku , walikubaliana kutoamsha magari yao siku inayofuatia kutoa madai ya kuyanyaswa na Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kwa kutozwa faini kubwa pasipo kuwa na makosa ya msingi. 
  Kufuatia mgomo huo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amewataka madereva wa daladala waliogoma kusafirisha abiria katika Manispaa ya Morogoro kusitisha mara moja mgomo wao na kurejea kazini. 
 “ Leo asubuhi kumekuwa na mgomo wa daladala za mjini Morogoro , wao wanawalalamikia askari wa Usalama Barabarani kwa kuwa wanawapiga faini kubwa kutokana na makosa ya magari barabarani” alisema Kamanda Shilogile.
Akielezea kiini cha mgomo huo. Hata hivyo alisema haikuwa sahihi kwa wao kufikia hatua ya kugoma kuwa vile jambo hilo lilikuwa linazungumzika kwa kukutana kwa pamoja kupitia uongozi wao , uongozi wa Polisi na wa wilaya ili kujadili kile ambacho wanaona kinakwenda tofauti na utaratibu wa kisheria za usalama barabarani. 
 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Polisi wa Kikiso cha Uslama Barabarani wapo kwa ajili ya kudhibiti ajari za baranarani na kuhakikisha magari ya nayofanya kazi za usairishaji ni mazima na si mabovu. 
 “ Askari wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo za usalama barabarani...hawapo kumwonea mtu , kazi yao ni kukamata magari mabovu na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani na kupingwa faini kuligana na makosa yaliyojitokeza” alisema Kamanda Shilogile. 
Hivyo alisema magari mazima ambayo yamekidhi vigezo vya usafirishaji ndiyo yanatakiwa kuwepo barabarani, hivyo Jeshi hilo halitasita kuyakamata yale ambavyo hayajakidhi vigezo hivyo kwa kusingizio cha kuonewa. 
 Kamanda huyo aliwataka madereva ambao wanaona magari yao ni mazima na wanaonewa na Askari wa Usalama Barabarani wanao wajibu wa kuwasilisha malalamiko yao kwa viongozi wa Jeshi hilo ili yafanyiwe kazi . 
 Hivyo alisema , pale watakapobani kuna ukiukwaji wa utaritu na sheria kwa upande wa Askari hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa askari kulingana na kanuni za jeshi la Polisi nchini. Hivi alisistiza kuwa , kama magari yao ni mabovu na yanafanya kazi za kusafirisha abiria , ni wajibu wa Askari wa Kikosi cha usalama barabarani kuyakamata na kuyapiga faini bila ya kumwonea mtu. Kutokana na mgomo huo wa muda ,viongozi wa chama cha madereva wa daladala, Uongozi wa Serikali ya Wilaya , Sumatra pamoja na Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro walikuwa na kikao cha pamoja kwenye Ofisi y Mkuu wa Wilaya ya Morogoro kulipatia ufumbuzi wa suala hilo. 
 Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Morogoro wakiwemo na wanafunzi walilazimika kutumia usafiri wa magari madogo ya wazi ‘ Suzuki’ na wengine kupanda Pikipiki’ Bodaboda’ na kila aina ya usafiri ili kuwahi kwenye shughuli zao. 
Mbali na kundi hilo kutumia usafiri wa aina hiyo, wananchi wengine waliamua kutembea kwa miguu wakiwemo wanafunzi , ambapo wenye magari madogo walionekana kufurahia hali hiyo wakisema wamejipatia kipato kizuri za kuendesha maisha yao kwa siku hiyo. 
 Hata hivyo baada ya mazungumzo ya pande hizo , madereva hao walirejea barabarani kuanzia saa kumi jioni ya Machi 19, mwaka huu kuendelea na kazi ya usafirishaji wa abiria
Kufa kufaana. Magari madogo yakisanya baada ya daladala kutokewa barabari kufuatia mgomo huo

Kila aina ya usafiri ulitumika
Wengi waliamua kutembea
Wanafunzi katika lori
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustine Shilogile

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tokeni huduma kwa wananchi, mnataka polisi wayafumbie macho makosa yenu?Na kama vipi muyaondoe kabisa waje watu wanaoweza kufanya biashara huku wakizingatia sharia.

    ReplyDelete
  2. Nahisi huyo mkuu wa usalama Morogoro hajasoma Alama za Nyakati-na atang'oka kitini punde tu.Yaani watu wazima na akili zao waache kazi ya kipato bila sababu za msingi?Bw.Shilogile,mtie hatamu ya ulimi huyo RTO wako mapema,atakutia ktk matatizo.Tz ya leo ni ya kidemokrasia.

    ReplyDelete
  3. hatari kwa usalama wa raia.

    ReplyDelete
  4. Hapana chezea sisi bebe! Bado Dar sasa.

    ReplyDelete
  5. Serikali inashikwa pabaya. Falsafa ya ikiniacha umeniogopa ukiniadhibu umenionea. Hatujazoea kutii sheria bila shuruti, pia tatizo ni mazoea na ukicheka na kima.... utavuna mabua. Dala dala wanataka wafanye watakavyo kama vile serikali hakuna.

    ReplyDelete
  6. RUSHWA, RUSHWA, RUSHWA..... NDIO TATIZO KUBWAAAA....

    Kwani nini hizo faini hazina RISITI!!! Mbona Trafiki anakuandikia ulipe fasta wakati yeye mwenyewe hana risiti kama uthibitisho??? why..

    Hili jeshi linatakiwa kusafishwa, na kama kweli ndio mnawapatia vijana wenu hivyo vitabu watafute hela kwa nguvu NO No No. haya magari hatukununua woteeee....

    Nakumbuka enzi za mwl. baba zetu hawakuwa na VITAMBIiii... Turudishe nidhamu jamani, Askari mnyenyekevu na mwenye nidhamu hauwezi kuwa na KITAMBI. Je! paredi za asubuhi, mchakamchaka, n.k. Askari anatakiwa awe fit wakati wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...