Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Asante Bwana Kaka Michuzi, ngoja tusikilize hii hutuba ya masaa mawili kabla ya kutoa mrejesho.

    Mdau
    Diaspora North America.

    ReplyDelete
  2. Teh teh teh teh.....mwani , karafuu na kombe za pwani....

    ReplyDelete
  3. kutowazungumzia wazee wetu waliotutangula ni ujinga na kutojuwa tunapotoka hatupajuwii tuwape heshima yao kabisa,wazee wetu hao.
    big dad

    ReplyDelete
  4. Kazi bado mbichi!! Hivi wakati anaongelea Wapemba kuwa na ardhi kubwa tu kule kwa Mh. Simbachawene, mbona hakugusia jinsi ambavyo wa-Tanganyika hawawezi au hawaruhusiwi kufanya vivyo hivyo kule Zanzibari? Nafikiri swala la umilikaji wa ardhi ni kubwa mno kuliko hata hizo kero nyingine, kwani ndo maana hata EAC kwa wa-TZ imekuwa tete kwa ajili ya swala la ardhi!

    ReplyDelete
  5. Hivi Rais hakupata kutoa maoni yake kwa Tume ya mchakato wa kutengeneza rasimu?

    ReplyDelete
  6. Namshukuru mweshimiwa rais kwa kutupa darasa la kuhusu muundo serikali wengi wetu tulikuwa washabiki bila kujua ukweli. Big up Mr president.

    ReplyDelete
  7. Nimekuelewa Mheshimiwa Rais, kuwa huna tatizo na mapendekezo yoyote ambayo Bunge Maalum wataweka kwenye KATIBA INAYOPENDEKEZWA, so long as wafanye "informed decisions". Waisome Rasimu neno kwa neno, Ibara kwa Ibara, Sura kwa sura, nukta, koma etc.

    Lakini kila watakachokipendekeza kiwe kinatekelezeka. Wakipendekeza Serikali tatu au mbili basi waziwekee MISINGI MADHUBUTI ambayo itafanya muundo utakaopendekezwa utekelezeke ili tusiingie kwenye matatizo.

    Hii ndio tafsiri yangu.

    ReplyDelete
  8. Hotuba bila shaka imewaingia wengi walioisikiliza na hata wale vichwa ngumu nao tabaan wamepata tafakuri kubwa. Cha msingi sasa ni kwa Wapemba kuanza kuhamisha rasilimali zao walizowekeza Tanganyika zinazohamishika kupeleka Pemba vinginevyo sidhani kama Watanganyika wataendelea kukubali Wapemba kuendelea kubakia kwao wakifurahia maisha waliyonayo baada ya mageuzi ya kisiasa yanayotarajiwa na kupigiwa debe na Wabunge wengi hasa wa kutoka Pemba. Naamini athari itakayoletwa na matokeo hayo itakuwa sio kubwa kwa Wazanzibari wa Zanzibar (Unguja) kwa vile wao hawana tabia ya kuhama kwao na kuhamia mbali.
    Ninavyoona in the long run hata sisi Waunguja tutawataka Wapemba wafanyie shughuli zao Pemba kwani hata nafasi za kulima na kuzikia watu hapa Unguja zimeadimika kwa kufanywa makaazi na jamaa kutoka Pemba hali ambayo hata Waunguja wengi hawafurahishwi nayo!!!!! Pia labda hizi fujo za kijinga ambazo ukizichunguza kwa makini utaona kuwa chanzo ni ndugu zetu kutoka Pemba; italeta afueni kidogo kwa Wana Unguja iwapo pia zitahamia Pemba ili nao waonje consequences za purukushani za vijana wao.
    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  9. Maneno ya anony wa 8 ni ya ukweli mtupu, Wapemba tunao hata kijijini kwetu Kiombo. Napatwa na mshangao kwa vijana wetu kuhamia mjini Singida kwa wingi na nafasi zao zinajazwa na hao ndugu kutoka Pemba. Kwa kweli ni vijana majasiri na ni watafutaji hasa, ila ninawaomba wawe na hisani na utu kwa sisi wenyeji wao kwani mambo yakigeuka hakika mali zao tunarithi tena bila ya kuchelewa.

    ReplyDelete
  10. Tatizo ni kuwa huu mchakato unahitaji misingi ya elimu ya sheria na kuwa na taarifa sahihi. Nampongeza kwa kuagiza isomwe neno kwa neno, mstari kwa mstari, aya kwa aya nk... Hiyo ndiyo kwenye lugha ya kisheria inaitwa ku peruse lakini wabongo tumegeuza kuperuzi ni kukupitia juu juu ovyo onyo. Nimeona wengi wamemchukia kwa kupasua ukweli na wanavutwa na hisia zao binafsi. Tuache busara itawale. Ila hata mimi nakwazwa na hili la wabara kunyanyapaliwa visiwani na wavisiwani kushika wizara hata zisizokuwa za muungano.

    ReplyDelete
  11. achane lukha za kibaguzi na nyinyi tafuteni mtapata sio choyo wazanzibar wakidai muungano wa usawa mnawataja wapemba maana mna chuki nao na mkianza zambi hiyo hamtakuwa salama maana kuna wapemba wameoa watu wa bara na wana watoto wakubwa na wabara wameoa wapemba sasa nyinyi yapalilieni

    ReplyDelete
  12. wapigaji debe wa vyama vya siasa basi sasa kaulizeni wananchi wanataka nini yaani kura ya maoni wanachotaka ndio wapewe kwani hii nchi ni yao sio ya chadema wala ccm hili hapa Tanzania ndio tatizo.

    Rais ana haki ya kutetea muundo anaoupenda yeye na wa chama chake hiyo ni haki yake na ni vema aseme hivyo sasa nimeelewa kwa nini ccm walitaka aje warioba kwanza kisha afuate rais kwa sababu hawakutaka aje rais kwanza kabla hajapata nakala ya hotuba ya warioba na kuja kuichambua anavyoona yeye.

    pia kwanza kabla ya kwenda kwa wananchi wenyeviti wa vyama vya siasa wote wapewe muda sawa wa kuja kupigia debe mifumo wanayoitaka na wao ya binafsi na ya vyama vyao kama aliopewa mwenyekiti wa ccm.
    kupiga debe kusiwe kwa ccm tu hapo ndio ninapowaona hawa si waungwana.
    muungano wa serikali ninaouona mimi unafaa ni ule wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar kama mbili ndio hizo basi sawa lakini kama mbili zenyewe ni zile za zamani yaani Zanzibar na muungano huo si muungano ni usanii wa 1964 unaendelezwa.
    Hamna uboreshwaji wala kuondoa kero ikiwa miaka 50 hamkuondoa kero mnahitaji 50 mingine uhai wa mtanzania ni miaka 42 tu kwa mujibu wa sayansi sasa uboreshaji mwingine tukaushuhudie makaburini?

    Tanganyika imeuwawa kwa makusudi na hilo ni kosa na shauri la waliouwa Tanganyika sasa baadhi ya wakereketwa wa ccm wana hamu ya kuiuwa na Zanzibar kwa kisingizio cha kuwa Tanganyika imeuwawa.
    Umeona wapi mtu akauwa mwanae kisha akaenda kupiga hodi nyumba ya pili kwa jirani kumuomba kwa hisani yake na yeye amuuwe mwanae ili waweze kuishi kwa salama na amani kwa vile wanaishi mtaa mmoja{Tanzania}

    Ndio maana ukaona Zanzibar haikuwahi kufa wala haitokufa kila siku wanaiboresha Zanzibar yao kwa kuibadili katiba yao na kuitambua kama nchi, kwa sababu mauaji ya Tanganyika yamefanywa na watanganyika sasa msilaumu nchi jirani kwa kosa la marehemu huyu.
    mdau.
    Windhoek, Namibia.

    ReplyDelete
  13. kwani nani kasema muungano ukivunjika wapemba warudi kwao , au watanganyika warudi kwao? huu ni upungufu wa fikra, kwani hapa tanzania bara/ zanzibar hatuna watu wa mataifa mbalimbali wanaishi na kufanya kazi zao? sasa kwa nini wapemba wasiweze tanganyika , au watanganyika wasiweze kule zanziba? tena bado watu hawa wamechanganya damu kwa hio muungano wa serikali ukifa sio tatizo hata kidogo , muungano wa damu utabakia

    ReplyDelete



  14. Mr. President, WHY DID YOU SEE MORE OF ISLAND THAN MAILAND .. TUMEKUKOSEA NINI BABA? TUNAOMBA TUPEWE TUNACHOOMBA ...NYINYI BAKINI NA SIASA ZENU ZA KIPWANI.

    ReplyDelete


  15. WALE WAPEMBA WA MPWAPWA WAMEKOSEA ... KULE NI KWA WAGOGO , NA WATANGANYIKA WENGINE ...

    ReplyDelete

  16. Wapemba Hongereni sana kwani hii katiba ni kwa ajili yenu tu

    ReplyDelete
  17. Afadhali Mkuu JK, umewapa mwanya wa kupumua jamaa wanaopigania uraia pacha. Maana kuna jamaa wamejipa madaraka ya kuwakatalia uraia ndugu zao kwa ubinafsi wao humu kwenye mitandao. Narudia tena, pigeni kelele sana, lakini wakuu wamepanga tayari kuhusu ili swala au swala la serikali la 2 na litakuwa hivyo. Wakati utasema, msema kweli ni nani!? Naamini Chochote kinawezakana, msikatee tamaa jamaa wa uraia pacha tupo pamoja.
    Mmbongo Chiberia.

    ReplyDelete
  18. Tutakapogawana watoto wataamua wapi kwa kuelekea kwani si hata kwenye ndoa za dini tofauti watoto huegemea upande fulani wa imani? Itakapotokea uwekezaji kwa wasio wazawa utaangaliwa tofauti na likely treatment itakayotolewa ni ile ya raia wa kigeni, si ndio maamuzi ya kidemokrasia? Nilazima na athari zake nazo zibebwe.

    ReplyDelete
  19. Ikiwa Zanzibar ni mzigo kwa Serikali ya Muungano, basi iwachieni ijiendeshe wenyewe na iwe na mamlama yake, kwanini mmeishikilia tu, na hii nchi si ya Rais Kikwete wala Rais Sheni, wenyewe ni wananchi, na wananchi ndio wa kuulizwa mabadiliko gani yafanyike.... usilazimishe vitu wananchi wengi hawataki... huo ni udikteta.... Tanganyika wanataka Serikali yao, waachiwe wapewe, na Zanzibar wanataka Mamlaka kamili kama Nchi ya Zanzibar basi waachiwe wenyewe.

    ReplyDelete
  20. Salama aleykum Bwana.MICHUZI. Mimi ninahisi hawa wajinga wanaoandika coments za kibaguzi ilikuwa kwa heshima ya Blog yako na wengineo zilikuwa hazina maana ya kuzichapisha na watu kusoma mambo kama hayo. Wanawazungumzia WAPEMBA Kuhama na kurudi makwao PEMBA huo ni ujinga na choyo cha roho tukumbuke kuwa Wapemba hawakuzaliwa Matajiri ni akili zao, Kujituma kwao, na kusoma. Sasa hawa nduguzetu wengine kusoma hawataki kujituma wao kwao ni tabu na wanahisi utajiri unaweza kuupata bila ya kuhangaika,Tukumbuke hata Marehemu waziri kiongozi DR.OMAR ALI JUMA.M/Mungu amrehemu alisema Wapemba wanajituma na sisi tusikae vibarazani tuu na kulegeza midomo tukategemea serikali tuu ni lazima tujitume na tuhangaike . Mimi ninawaambia tu kwanza wapemba hawaoni tabu kurudi makwao na kama utaangalia na kuchunguza utaona Wapemba wengi wanajenga makwao na wanaekeza makwao na hawa watu wenye matatizo ya kibaguzi na wapemba wasiwe na wsi wasi kwa sababu wengi wao wanategemea riziki zao kwa kutumwa na hao hao WAPEMBA .mimi ninahisi tuwe na hadhari nini cha kuzungumza na tusizungumze tu kwa chuki binafsi kwa sababu nitatoa mfano mdogo tuu ukiangalia ndugu zetu wa KIMAKUNDUCHI wengi hawakusoma na ndio maana wengi wao kazi yao kubwa ni kujiunga n jeshi la POLISI ukienda huko Pemba wameja wamakunduchi wameowa WAPEMBA wameshazaa nao watoto na hakuna mpemba anayewabuguzi wala kuwatia midomono kila mtu na rizki yake na sio wamakunduchi tuu na wengine wengineo ambao hawana asili na kisiwa cha PEMBA hata ndugu zetu wa Tanganyika wapo Pemba na wala hawana nia ya kuhama sasa jee wapemba na wao waanze kukaa tayari . Na wapemba walioko hapo unguja sio hao tuu au hapo Tanganyika Wapemba wapo kila pembe ya dunia Kenya ,South Africa Uganda, London,America, Dubai Oman na nchi nyingi tuu na hakuna anae wataja wala kuwabughuzi wanafanya kazi zao ilimradi hawavunji sharia tuu ,Wascotish mwezi ua NOVEMBER wanapiga kura ya maoni kama wanataka kubaki UK au laaa Na hakuna mtu aliyetamka wahame ENGLAND ua vyenginevyo sisi tayari tunaaza upuuzi wa kuwabaguwa WAPEMBA mimi nahisi cha msingi sio kuwachukia WAPEMBA isipokuwa ni kushindana na kuiga nini WAPEMBA wanafanya na kufanikiwa kimaisha na sio kuanza fikra za kijinga na kibaguzi hazitotusaidia lolote isipokuwa kutuzidishia umasikini.

    ReplyDelete
  21. maneno murua hayo juu kwa wenye kutafakari , mwenyezi mungu anasema kuna waja wake amewafadhilisha zaidi kuliko wengine na hio ni mipango yake mola , hakuna haja ya kuoneana choyo,
    Krimea tayari washapiga kura na washaamua kuwa na urusi , angalieni demokrasia hio , haikuchukua hata mwezi , sisi miaka 50 tunataka tuachiwe zanzibar yetu mpaka leo wametuganda kama urimbo

    ReplyDelete
  22. "Alichosema Rais ni maoni yake binafsi na chama chake. Ningemshangaa kama angesema tofauti na msimamo wa chama chake" by Askofu Dkt. Shao. Amenifurahisha sana huyu Askofu kwa kusema ukweli kwamba alichosema Rais ndio msimamo wa chama chake asingeweza kusema tofauti wanachama wake wangemshangaa na sio maoni ya watanzania wote. maoni ya watanzania wote yako kwenye Rasimu siyo kwenye hotuba ya Rais. Yeye ni Mwenyekiti wa chama hiyo inajulikana wazi na ndio maana ameshindwa kujibu masuala ya Zanzibar kuvunja katiba na kujitoa kwenye muungano, na walivunja wao kama chama wakiona lakini wakanyamaza leo ndio wanasema watarekebisha vipi? Mie binafsi nataka muungano wa serikali moja ambalo ndio lengo la baba wa taifa Zanzibar iwe mkoa ndani ya Tanzania ili kweli tuitwe watanzania kuliko ilivyo sasa kuna watanzania na wazanzibar lakini hata ccm kinapingana na sera za mwalimu kwa kung'ang'ania serikali mbili, hizo mwalimu aliweka za mpito tu kuelekea kwenye serikali moja. kama hiyo ikishindikana nataka serikali mbili lakini Tanganyika iwe na mamlaka yake na Zanzibar iwe na mamlaka yake na ikishindikana hiyo basi tuwe na mfumo wa nchi moja serikali mbili kama walivyotuachia waasisi lakini kuwe na marekebisho safari hii Zanzibar ndio iwe ndani ya muungano Tanganyika iwe nchi kamili na bendera, wimbo wa taifa etc. kama ilivyokuwa kwa zanzbar kwa maiaka 50 iliyopita.

    Tunaomba wajumbe wazingatie maoni ya wananchi na sio maoni ya Wenyeviti wa Vyama, na pia wasome nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa na Tume kama ushahidi wa kilichosemwa na tafiti mbalimbali zilizosomwa, msiwe wavivu kusoma ili mfikie maamuzi yenye busara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...