Kamanda wa polisi mkoa wa
Njombe SACP Fulgence Ngonyani
Na Edwin Moshi, Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  imesema kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi, ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki.

Tukio hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta mkoani Mbeya
Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo. Chanzo bado hakijafahamika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...