Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mheshimiwa Mbarouk Nassor Mbarouk, tarehe 02/03/2014 aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum, Makamu wa Rais UAE, Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai, jijini Abu Dhabi, UAE. Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Kasri ya Al Mushrif, zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa UAE.
Balozi wa Tanzania nchini UAE, Mheshimiwa Mbarouk Nassor Mbarouk na Mkuu wa Itifaki wa UAE, Mheshimiwa Shihab Al Faheem (kulia) wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa.
Mheshimiwa Balozi akiwasilisha salaam kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Tanzania na kujitambulisha rasmi.
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum, Makamo wa Rais wa UAE, Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai, kwenye kasri ya Al Mushrif, mjini Abu Dhabi, UAE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mbarouk nakukubali. Kwa uchapaji wako wa kazi sitoshangaa ukawa raisi miaka ya baadae labda mafisadi awakupinge tu...

    ReplyDelete
  2. Chuwa-Tokyo JPMarch 05, 2014

    Huyu Mh Mbarouk ni kiongozi mchapa kazi sana.Namfahamu vizuri sana toka akiwa kaimu balozi kule Moscow- Russia alipigania na kutetea sana haki zetu tuliokuwa tunasoma nchini Urusi wakati ule.Hakika anastahili nafasi hiyo na anafaa sana hata kuwa Rais wa Tanzania miaka ijayo.
    Mwenyezi Mungu akubariki sana Mh.Mbarouk na azidishe matunda ya kazi zako mara dufu.
    HONGERA SANA

    ReplyDelete
  3. Hongera sana kaka Mbarouk pia Hongera Balozi Jaka Mwambi kwa Kututengenezea Balozi Mpya Kutoka kituoni kwako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...