Bendi pendwa ya African Stars “Twanga Pepeta” mwishoni mwa mwezi huu itafanya ziara ndefu ya maonyesho katika mikoa ya nyanda za juu kusini. 
 Twanga Pepeta itaanzia ziara yake NJOMBE siku ya Jumatano tarehe 26-03-2014 katika ukumbi wa Turbo.
 Siku inayofuata tarehe 27-03-2014 siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza kabisa watakuwa Wilaya mpya ya MBABABAY katika ukumbi wa BAY LIVE SOCIAL HALL. 
 Ziara ya Twanga Pepeta siku ya Ijumaa tarehe 28-03-2014 itahamia Songea mjini katika ukumbi wa Serengeti. 
Siku ya Jumamosi tarehe 29-03-2014 itakuwa ni zamu ya Jiji la Mbeya katika ukumbi wa City Pub. Maandalizi ya ziara yanaendelea vizuri na Twanga Pepeta imejitayarisha vilivyo kukonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza katika maonyesho yake. 
 Twanga Pepeta itatumia ziara hii kuitangaza albamu yake mpya ya Nyumbani ni Nyumbani pamoja na kupiga nyimbo zilizopo kwenye albamu zake 12.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wazalendo wa Twanga pepeta kamataieni kasi hiyo hiyo,tangazeni muziki wa dansi mpka mikoani
    wadau
    FFU-Ughaibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...