Mwenyekiti wa  Benki ya  Covenant  Balozi Salome Sijaona  akimkabidhi  mratibu wa uhamasishaji wa vikundi vya Wilaya ya Temeke Bi.Tukae Kondo ufunguo wa pikipiki baada ya kuwapatia mikopo wajasiliamali mbalimbali.Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi imewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo na mitaji. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa  benki ya Covenat  Sabetha Mwambenja, akiwasisitizia  jambo juu  ya kurejesha mikopo baadhi ya wajasiriamali waliopata mikopo  ya pikipiki  iliyotolewa na Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasilia mali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo . Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Balozi Salome Sijaona
Mwenyekiti wa  Benki ya  Covenant  Balozi Salome Sijaona  akimkabidhi  Mwenyekiti wa Kikundi cha Mshikamano cha  Yombo Vituka cha jijini Dar es Salaam,Charles Rweyemamu  ufunguo wa gari aina ya basi lenye thamani ya shilingi Milioni 45 .Benki hiyo kwa kushirikiana na umoja wa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi wamewawezesha wajasiriamali wadogo nchini kwa kuwapatia mikopo. Hafla hiyo imefanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Covenat bank Sabetha Mwambenja.
 Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Covenant  Sabetha Mwambenja akiongea na Waandishi wa habari  juu ya benki hiyo kutoa mikopo kwa wajasiliamali wadogo  nchini  ili waweze kujikwamua  kimaisha kwa kuwapatia mitaji  ambayo ilijumuisha  Basi la abiria ,pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jonathan UrasaMarch 19, 2014

    Hii Benki inakuja kwa kasi, na inaonekana ina lengo zuri la kuwainua wajasiriamali wadogo. Asante sana Covenant Bank.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...