Mkuu wa mkoa wa Mara Mhe. John Gabriel Tupa 
(pichani, enzi za uhai wake) amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tarime.  

Habari zilizothibitishwa zinasema Marehemu Tupa alianguka na kupoteza fahamu akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. John Henjewele,  alikokuwa akipokea taarifa kabla ya kufunga mafunzo ya mgambo wilayani humo.

Mara baada ya kuanguka juhudi za haraka zilifanyika za kumkimbiza hospitali ya Wilaya ya Tarime ambako alitangazwa kuwa ameshafariki mara alipofikishwa hapo.

Mwili wa Marehemu umepelekwa hospitali ya Mkoa wa Mara ili kuhifadhiwa wakati taratibu za m,aziko zikiandaliwa.

Tutaendelea kuwapasha kinachoendelea kwa kadri taarifa zitavyokuwa zikitufikia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. JAMANI ITS SO SAD
    HE WAS SUCH A NICE PERSON
    NAKUMBUKA NIKIWA KIKAZI DODOMA YEYE ALIKUWA NI MKUU WA WILAYA NA MKUU WA MKOA AKIWA LUKUVI JAMANI DODOMA WAS LIKE HEAVEN WALIKUWA SO WELCOMING UKIWA NA SHIDA
    APUMZIKE KWA AMANI

    ReplyDelete
  2. Inna Lillah wa inna ilayhi rajiuun
    HAKIKA SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE SOTE TUTAREJEA. NA PINDI ITAKAPOFIKA SAA, MAUTI YATAMKUTA YEYOTE MAHALI POPOTE ALIPO BILA HATA YA TAARIFA. HATUNA BUDI KUJIANDAA NA MAISHA BAADA YA MAISHA YA HAPA DUNIANI KWA KUJITAHIDI KUTENDA MEMA NA KUACHA MABAYA.

    ReplyDelete
  3. R.I.P John Tupa. Alishawahi pia kuwa mkuu wa wilaya ya Chunya. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen.

    ReplyDelete
  4. mwenyeenzi mungu ailaze roho ya marehemu mahala panapo stahili...namkumbuka vizuri kipindi akiwa ni mkuu wa wilaya ya MWANGA mkoani kilimanjaro he was a leader.

    ReplyDelete
  5. RIP Baba

    ReplyDelete
  6. So sad,May he lay in Peace

    ReplyDelete
  7. The mdudu,huu ni msiba wetu sote watanzania poleni sn wanafamilia inasikitisha kuona mwezetu hatoiona katiba yetu mpya itakayokuja mwenyezi mungu mwema wa rehema akupokee kwa mikono miwili na mbele yako nyuma yetu hii safari ni ya kila mwanaadam hapa duniani.

    ReplyDelete
  8. Tulikupenda kwa kazi yako,ila mungu anakupenda zaidi

    ReplyDelete
  9. Sisi sote ni waja wa ALLAH na kwake yeye tutatejea

    ReplyDelete
  10. Oh Brother John Tupa, nisemeni nini? Eh Mwenyezi Mungu, tumwomboleze vipi Muungwana, Mchapakazi, Kiongozi na Binadamu huyu! Umemchukua ghafla, akichapa kazi, kazi njema aliyoipenda na kuitekeleza kikamilifu - kutumikia uliompa, bila kuchoka na kwa upendo, hekima na heshima kubwa. Ee Mwenyezi Mungu uliye asili ya yote mema, mpatie pumziko la milele kwako, Amina.

    Mrs Tupa, shemeji yangu, pamoja na wanenu, Mwenyezi Mungu awafariji, awawezeshe katika kipindi hiki kigumu. Poleni sana, tunawapa pole sana.

    Balozi Dr. James Alex Msekela
    Roma, ITALIA

    ReplyDelete
  11. Mwenyezi Mungu aistiri roho ya marehemu pahali pema panapostahiki ,Mengi mazuri yamesemwa juu ya Hon John G Tupa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...