Bunge nchini  Kenya limepitisha sheria inayomruhusu mwanaume kuoa wake wengi atakavyo, na halazimiki kumshauri mke wake juu ya uamuzi huo.
Katika marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya Kenya yaliyopitishwa Alhamisi iliyopita, hata hivyo ndoa zote zitatakiwa kusajiliwa na umri wa chini  wa mwanamke kuweza kuolewa umewekwa ili kuzuia ndoa za mapema  za watoto, hasa wasichana.
Siku hiyo ya Alhamisi Wabunge wote wanaume, ambao ni wengi, waliunga mkono kuondolewa kwa kipengele katika Sheria hiyo ya Ndoa kilichomtaka mwanaume afanye mashauriano na mkewe kwanza kabla ya kuoa mwanamke mwingine.
Wabunge wanawake waliolaani hatua hiyo walikuja juu na kususia kikao kwa kutoka nje wakidai Sheria hiyo haiwatendei haki wanawake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. So very STUPID law, what message are they sending to the young girls and boys, what about allowing a woman to marry several husbands.
    UKIMWI afilika hautaisha kamwe,

    ReplyDelete
  2. SHERIA HAIWATENDEI HAKI WANAWAKE WALIOKO KWENYE NDOA LAKINI INAWATENDEA HAKI WALE WASIOKUWA KWENYE NDOA NA WANATAKA KUOLEWA HATA KAMA NI MKE WA PILI.

    NGOJA NIFANYE JITIHADA NIHAMIE KENYA.

    ReplyDelete
  3. Watumwa wa wazungu. Yaani kwa sababu mzungu ataka mke mmoja basi na sisi weusi lazima iwe hivyo.

    Sisi tuna tamaduni mila na desturi zetu bwana.

    Nyie kina clementina endeni huko, sis Lawino watutosha.

    ReplyDelete
  4. KENYA SI NCHI YA KIDINI

    kwenye nchi ya kisekyula sheria ya mke mmoja (ya kikristo) haitakiwi ifatwe na wasio wakristo (wakabila na waislamu). Na mkristo ana haki ya uhuru wa kuoa mke mmoja halazimishwi kuoa wengi.

    Nadhani haki imetendeka.

    ReplyDelete
  5. kwenye dini yetu ya kiislam mwisho wake wane sasa Kenya mbona hamjatuwekea wazi mwisho wake wangapi kuowa bila kushauriana wa mama watoto.
    kama zaidi ya wanne basi mtuletee habari upesi tupate kuhamia huko kwani hawatutoshi lakini katika dini sio katiba hamna mabadiliko.

    ReplyDelete
  6. HAPO WAKENYA KWELI WAJITAMBUA; HAWATAKI KUBURUZWA NA WAKOLONI. KWA MWENDO HUU MTAENDELEA KWA KASI, MUNGU AWASAIDIE. NA SASA MUNAJUA NINI MAANA YA KUWA BINADAMU, AHSANTE SANA

    ReplyDelete
  7. Hawa warukia mambo wanachosha sana!!... hivi mmeelewa vizuri?? swala sio udini hapa, swala ni mwanaume kuongeza mke bila kushauriana na mama watoto kama ilivyokuwa awali, au??

    ReplyDelete
  8. Hiyo ndiyo haki, kama alivyosema anony hapo juu "HAKI IMETENDEKA"

    ReplyDelete
  9. MKE WA MWANZO ASIULIZWE BALI ATAARIFIWE.

    yaani mke wa kwanza akikataa basi jamaa asioe?

    ReplyDelete
  10. Swala hapa ni 'bila kushauriana na mkewe" ina maana polygamy ilikuwa inaruhusiwa toka zamani isipokuwa kwa ruhusa ya mke.
    Haki za wanawake hapa hazipo / zimevunjwa.
    Je mwanamke ana haki kuwa na uhusiano nje ya ndoa?
    tusubiri katiba mpya ya Tanzania itatoa haki zipi kwa wanawake wa Tz,au watabakia kuwa "second class" kwenye sosait yetu?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...