Mgombea Ubunge Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa na wafuasi wa chama hicho jana usiku katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa baada kutangazwa matokeo ya awali yasiyo rasmi .Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na ushindi wa kishindo kwa kushinda kata zote 13 zilizoko kwenye jimbo hilo la Kalenga.
======= ===== =======
Matokeo ya Uchaguzi Mdogo jimbo la Kalenga Iringa vijijini yametangazwa rasmi jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mjini Iringa,kuwa chama cha CCM kilipata jumla ya kura 22962,na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Kilipada idadi ya jumla kura 5853 na chama cha CHAUSTA kilipata kura 150.Hivyo chama cha CCM kilishinda kwa asilimia 79.4,CHADEMA asilimia 20.1 na CHAUSTA asilimia 0.5.Matokeo hayo ni ya jumla kwa Kata 13 za jimbo hilo.
hongera mgimwa
ReplyDeletePamoja na ushindi wa kisiasa wa Godfrey nadhani pia italeta faraja ya namna fulani kwa familia ya Mgimwa....unajua, mimi si sana kama sisiemu ila kwa sababu hiyo tu (faraja kwa familia) nilitaka kijana ashinde hako ka-uchaguzi kadogo ....nadhani wadau watakuwa wamenielewa....However, bwana mdogo piga kazi sasa next election hutapata watu waku-sympathy na wewe watu wataangalia output...so make use of the opportunity watu waone uwezo wako wakupe kura za ukweli hapo 2015.
ReplyDeleteHongera mbunge mpya kijana, kazi sasa ni kuongoza jimbo na kuhamasisha maendeleo zaidi Kalenga.
ReplyDeleteWaliojiandikisha daftari la mpiga kura ni 71,000.
ReplyDeleteWalijitokeza kutumia haki yao ya kupiga kura ni 29,000.
Walioshindwa kujitokeza kupiga kura ni 42,000.
Asilimia ya waliojitokeza kupiga kura ni 29,000/71,000= 40.8% ya wenye haki ya kupiga kura.
Asilimia ya walioamua kutopiga kura ni 42,000/71,000= 59.2%
Inakuwaje wapiga kura zaidi ya asilimia 59% ya walio ktk daftari la mpiga kura wakae nyumbani na wasijishughulishe na haki yao hii ya msingi?
Tume ya Uchaguzi, CCM , CDM n.k wajiulize, kwa nini wananchi wanamua kukaa nyumbani na kususa kutumia haki yao ya kuchagua viongozi?
Mdau
Habari+ Data