Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema taifa, John Heche, akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lumuli, wakati wa kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia chama hicho, Grace Tendega uliofanyika kijijini hapo jana.

 Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo, akimwelezea mtoto Zakina Miwela, anayesoma darasa la pili katika Shule ya Msingi Lumuli, ambaye ni mtoto wa kiongozi wa CCM wa kijiji hicho, anavyoonekana bila viatu na sare zake kuchanika, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.
 Meneja wa Kampeni za mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Alphonce Mawazo na mgombea, GraceTendega, wakizungumza na akinamama wa kijiji cha Lumuli, katika kikao maalumu baada ya mkutano wa kampeni, zilizofanyika kijijini hapo jana.
Mgombea  wa CHADEMA akipokelwa Lumuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sio sawa kumdhalilisha mtoto..

    ReplyDelete
  2. Ebo!

    Siasa zingine jamani?

    ati mtoto wa Kiongozi wa CCM hana viatu na Sare za Shule, sasa kwa nini ninyi Chadema msiwajibike kumnunulia ?

    ReplyDelete
  3. Kwa mtaji huo Chadema Mmefilisika hamna busara wala akili mpaka mna mzalilisha mtoto,kukosa kwake viatu hakuhusiani kabisa na uongozi wa baba yake kuwa CCM,Sugu mbunge Mbeya watoto wangapi wanaishi mazingira magumu na viatu hawana hamjaliona hilo au wabunge wangapi wa Chadema wame nunua viatu na sare za shule kwa wtoto wa jimbo lao? Chadema mjipange jimbo la kalenga mshalikosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...