Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akizungumzia juu ya mradi ambao German wameshirikiana na Chuo cha VETA nchini katika kuhakikisha wanaboresha maswala ya elimu ya vitendo Tanzania. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru.
Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar Es Salaam VETA, Bi Benadetha Ndunguru akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kutambulisha mradi wa ushirikiano kati ya Vyuo vya Ujerumani na VETA kwa wanafunzi wa Tanzania.
Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akiongea na waandishi wa habari wakati alipowatembeza kwenye moja ya karakana ambayo inatoa masomo kwa vitendo yaliyo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship" iliyopo katika Chuo Cha VETA kilichopo Chang'ombe jijini Dar Es Salaam.
Meneja Mradi wa "German Dual System Apprenticeship"(katikati) Martin Mac Mahon akiwaonyesha moja ya magari yaliyotolewa na Kampuni ya Noble Motors kwaajili ya Mafunzo ya Vitendo yaliyo chini ya Mradi wa "German Dual System Apprenticeship" kwa wanafunzi wa Chuo Cha VETA.
Wanafunzi wa Chuo Cha VETA wakiwa katika mafunzo kwa vitendo ambayo yapo chini ya mradi wa "German Dual System Apprenticeship" ambapo wanafunzi wanapata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo na kuunganishwa na makampuni ambao wanafunzi hao hupelekwa kwaajili ya mafunzo zaidi.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...