Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
Akisaini mikataba ya makabidhiano ya Trekta lililonunuliwa kupitia
miradi ya DADPS huku Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimahewa,Bw Ally Seif
Malongola akisubiri kusaini mkataba huo,
Akisaini mikataba ya makabidhiano ya Trekta lililonunuliwa kupitia
miradi ya DADPS huku Mwenyekiti wa kijiji cha Kilimahewa,Bw Ally Seif
Malongola akisubiri kusaini mkataba huo,
Trekta lililokabidhiwa kwa kijiji cha kilimahewa wilayani Ruangwa
Afisa Mtendaji wa kijiji cha kilimahewa,Bw Rajab
Mohamed akisoma taarifa fupi kwa mgeni rasmi kabla ya kukabidhiwa kwa
Trekta ,Kutoka kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Ruangwa,Silvanus
Kilowoko na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa
Reubern Mfune

Katibu Tawala wilaya ya Ruangwa Silvanus Kilowoko
akikabidhi Mikataba ya Trekta iliyonunuliwa na DADPS kwa Mwenyekiti wa
Kijiji cha Kilimahewa Ruangwa
akikabidhi Mikataba ya Trekta iliyonunuliwa na DADPS kwa Mwenyekiti wa
Kijiji cha Kilimahewa Ruangwa
======= ======= ======
Na Abdulaziz ,Ruangwa.
Wilaya ya Raungwa katika kutekeleza mpango wa kilimo kwanza
Inahakikisha wakulima wanapata mbegu na zana bora za kilimo ikiwemo
matrekta kwa wakati sambamba na kuwawezesha wataalam wa kilimo
kutembelea wakulima mara kwa mara kwa lengo la kutoa ushauri ili
kuboresha kilimo.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
Ruangwa,Reubern Mfune katika hafla fupi ya kukabidhi trekta kwa
kikundi cha wakulima wa kijiji cha Kilimahewa kata ya Nachingwea
wilayani humo Mfune aliwataka wananchi kuthamini na kutunza huduma za kijamii
zinazotolewa katika maeneo yao zikiwa ni matunda ya utekelezaji wa
mipango ya serikali ya kuwahudumia wananchi wake katika sekta ya elimu
Afya ,maji na Kilimo.
Akisoma taarifa fupi ya Halmashauri kwa Mgeni rasmi ambae Pia ni
Katibu tawala Wilaya ya Ruangwa,Silvanus Kilowoko, Mfune alibainisha
kuwa kupitia mradi wa DADPS Serikali imetoa fedha jumla ya shilingi
milioni 40 na wananchi wamechangia shilingi milioni 4.6 kwa ajili ya
kununulia trakta lenye thamani ya shs milioni 43.9 kwa lengo la
kutekeleza mpango wa kilimo kwanza na halmashauri ya wilaya Ruangwa
imechangia shilingi milioni 1.5 kwa ajili ya kusafirisha trekta hilo
lililonunuliwa Suma Jkt.
"KWA Kuwa dhamira ya serikali wakati wote ni kupeleka huduma za
kijamii karibu na wananchi kama tulivyofanya kwa wananchi wa kata hii
hivyo basi nawaomba jamii kutoa Ushirikiano kwa halmashauri na
kujitolea kuchangia maendeleo na kutumia fursa hii kulima kilimo cha
kisasa kwa kutumia mbegu bora na elimu itolewayo na wataalam wa
kilimo"Alimalizia Mfune
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya RUANGWA
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji hicho bw Rajab Mohamed kwa
niaba ya wananchi alitoa shukrani kwa serikali na kutoa wito wa
kuongezewa wataalamu wa kilimo ikiwemo upatikanaji wa pembejeo kwa bei nafuu ili kulima kilimo cha kisasa

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...