
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwa katika daraja la Chimate ambalo
mbao zake zimeoza na kupelekea kuhatarisha usalama wa watumiaji wa
Daraja hilo katika Wilaya ya Nyasa. Ametoa agizo kwa Meneja wa TANROADS mkoani humo kubadili mbao katika daraja la Mto CHIMATE haraka na kuweka kambi
katika daraja la Mto MBULI kufanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na
wananchi ili kujua tabia ya mto huo hasa wakati wa masika.
Kutokana
na Mvua kubwa zinazoelendelea kunyesha Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma
zimesababisha madhara makubwa katika vijiji viwili ndani ya wilaya hiyo
ikiwemo kuharibu mazao mashambani pamoja na kusombwa kwa daraja la mto
Mbuli katika kijiji cha Ng’ombo.Hali hii imepelekea wakazi hao
kupata tabu pale wanapougua huku wanafunzi wakishindwa kwenda shule kwa
muda wa mwezi mmoja na wengine mashamba yao kusombwa na maji.
Hali
hiyo imepelekea huduma za kijamii kuwa ngumu kufanyika ikiwa ni pamoja
na upande wa matibabu pamoja na mahudhurio ya watoto shule.
Pichani aliyesimama katikati ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwangu akiwa katika Daraja la kijiji
cha MBUI ambacho daraja la mto ng’ombo limesombwa na maji na kukigawa
kijiji hicho sehemu mbili, sehemu moja ikiwa inashule na sehemu moja
kukiwa na zahatari.
Pichani
ni dereva wa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma aliyejulikana kwa
jina moja la Komba akitoa msaada wa kuwavusha watoto wa shule katika
daraja la mto Mbuli ambalo nilamuda lililotengenezwa na wananchi wenyewe
wa kijiji cha Ng’ombo.
Kulia
ni mwenyekiti wa CCM Mh.Oddo Mwisho akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa
Ruvuma Said Mwambungu kuhusiana na Daraja hilo lilisombwa na maji.
Pichani
ni wakazi wa Kijiji cha Ng'ombo wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Ruvuma
Said Mwambungu ambaye hayupo pichani akiwataka wakazi ho kuwa na subila
katika ujenzi wa daraja hilo kutokana na Mto huo kuwa na tabia za
kuhamahama. Hivyo akatoa agizo kwa wataalamu kuja na kuweka kambi ili
kujua namna ya kuweza kuudhibiti mto huo usijeukasababisha maafa tena
katika ujenzi huo pale utakapotengamaa.
Katika
picha ni wakazi wa kijiji cha Ng'ombo wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa
Ruvuma ambaye hayupo katika picha huku wakiwa katika nyuso za majonzi
kutokana na mvua kusababisha uharibifu.(Picha zote na Demashones)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...