Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai, akiendesha Ibada bya Misa maalum ya Shukrani kufuatia kifo cha Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma (100), aliyeaga dunia Ijumaa ya tarehe 17 January,2014 katika hospitali ya Mount Ukombozi na kupumzishwa katika nyumba yake ya milele tarehe 19 January, 2014 katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar.
Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikishiriki misa maalum ya kutoa shukrani iliyofanyika mwishoni mwa Juma jijni Dar.
Mchungaji John Muhina wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Andrea la Magomeni Mwembechai akimrithisha kiti alichopenda kukaa marehemu wakati wa ibada za Jumapili kanisani hapo mmoja wa watoto wa Mzee Arnold Nkhoma Bw. Amos Nkhoma.
Familia ya Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma ikitoka kanisani mara baada ya misa maalum.
Bi. Usia Nkhoma Ledama akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na baba yake mkubwa Michael Nkhoma,(kushoto) na Mzee Aidan Nkhoma.
Familia ya Marehemu Mzee Arnold Kambonapani Nkhoma wakiwasha mishumaa kwenye kaburi la Mzee Arnold Nkhoma mara baada ya misa maalum ya shukrani iliyofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar. Kwa picha zaidi ingia hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...