Timu nzima ya Golden Bush Veterans ambao ndio Mabingwa wa Veterani Tanzania (Bara na Visiwani) watahamishia makali yao Kilombero mkoani Morogoro. Tutakapokuwa Kilombero Golden Bush Veterans tutakuwa na mechi moja ya kirafiki siku ya Jumamosi uwanja wa Ruaha dhidi ya Wenyeji wetu Kilombero Veterans yenye wachezaji wazoefu waliowika katika soka la bongo wakiongozwa Mustafa Hoza.

Golden Bush itaondoka Dar es salaam siku ya Jumamosi saa kumi na mbili asubuhi, na msafara utaongozwa na Waziri Mahadhi kama mkuu wa msafara akisaidiwa na Ali Othman Nucci mjumbe wa kamati ya utendaji na msemaji wetu upande wa Zanzibar.

Kikosi kizima cha wachezaji 25 chini ya mwalim Madaraka Seleman na nahodha Wisdom Ndlovu a k a Mwakalinga kimejiandaa vya kutosha kufanya maangamizi yatakoweka historia huko Kilombero siku ya tarehe 29 March 2014.

Kwakuzingatia umuhimu wa game hii, Golden bush tunaweka camp ya wiki nzima Bagamoyo ili kujiweka sawasawa kwa ajili ya game hiyo ya kukata na shoka.

Asanteni kwa kunisikiliza.
 Onesmo Waziri “Ticotico” 
Msemaji wa timu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...