Moja ya kero kubwa hapa Dar ni msongamano unaotokana na kutopangilia
miundombinu na huduma vizuri.
Kwenye magazeti ya siku za karibuni, imeripotiwa kuwa mpango wa kujenga
stendi ya mabasi yaendayo mikoani eneo la Mbezi Luis umekwama kwa sababu
eneo lile halifai kutokana na kuwepo mkondo wa maji.
Nimekuwa najiuliza kwa nini kujengwa stendi pale mahali hajapapimwa (hivyo
ni vigumu kujengwa huduma za mahoteli, nk na kumwaga maji taka)... wakati
mbele kidogo tu pale Luguruni kuna eneo kubwa limetengwa kuwa satellite city
na mpaka sasa limebaki pori?
Kujenga hapo stendi kuu ya mabasi ya mikoani
pamoja na soko kubwa la jumla kungetosha kuhamasisha uwekezaji ambao ndio
ungesaidia patumike kama kituo cha huduma kama ilivyokusudiwa na kupunguza
msongamano mji mkongwe wa Dar.
Dar City Council bado wanatafuta maeneo
kuweka hiyo stendi wakati Luguruni iko pori kubwa pale. Hata waliwahi
kutaka kujenga stendi ya muda pale Chuo Kikuu Dar.
Hivi humu hakuna anayehusika na haya mambo atuelimishe?
Mdau wa Mbezi
Mdau wa Mbezi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...