Mheshimiwa michuzi tunashukulu sana kwa kazi yako ya kutujulisha yanayoendelea TANZANIA leo naomba unipe nafasi niweke ya moyoni mwangu na maoni yangu kuhusu huu mstakabali wa kupata katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Mengi yamekuwa yakisemwa sana kuhusu hii katiba au ni muundo ghani wa muungano tunaoutaka,watu wengi na wana siasa wamesahu kwamba muungano huu na katiba hii ya zamani ndio umetufanya tuwe na undungu  na pia tuwe na amani mpaka hapa tulipo.
Watu wengine wameandika katiba baada ya kumwaga damu na nitatowa mfano Kenya,Rwanda,Uganda,Burundi na majirani zetu wa Congo je hawa wana siasa wa CCM,CUF,CHADEMA haya yote mnaonekana kwenye macho yenu na kwenye masikio yenu hamkuyaona au kuyasikia??

Wazee wetu waliotangulia walikuwa na nia nzuri sana lakini leo inaonekana ndoto zao zitakufa na Muungano wetu  ambao umetupa amani na maendeleo yetu tuliyonayo mpaka leo yako mashakani, kutokana na watu wanaosema wanawalilia waTanzania kumbe  ni watu walio na agenda ambazo ni za kutumikia vibaraka wa nje.
Ndugu WaTanzania tume ya Mzee Warioba ilifanya kazi imekusanya maoni yaliyotolewa na watu na hii aiweze kuwa ndio katiba ya watanzania bali ni maoni ya wananchi na mwongozo wa kuweza kuandika katiba ya waTanzania,na baadhi ya mambo yaliyowekwa mule ndani mengine ni mazuri na mengine nilazima yafanyiwe mabadiriko tupende au tusipende kwa mfano sijawahi kuona MP anakuwa na kikomo,ili nasema  USA,UK,ambao tunawaona ni kama mababa wa demokrasia hawana kikomo,pili Tanzania ina watu milioni 44 au tano itakuwaje bunge liwe na wabunge 75 ,kuna mambo mengi ya kujadili na siyo jambo la Muungano  pekee. Katiba ina mambo mengi jamani!
Ndugu Wa Tanzania Raisi ametowa maoni yake mazuri na kasoro zilizomo katika hiyo rasimu hakuja kuwafundisha hao wabunge au kuwaambia nini cha kufanya bali alikwenda kufungua bunge na kutowa maoni yake na kuwaachia nyinyi wabunge kazi ya kufanya  lakini leo nashangaa wabunge wa upinzani wameanza kusema maneno ya kuropoka ropoka mbunge aliye onysha amekoma na kutowa maneno ya busara ni Mheshimiwa Zito. Hongera ndugu Zito.
Ndugu Watanznia napenda kuwaomba hawa wabunge tumewatuma kutupatia katiba na siyo maneno tunataka katiba ya watanzania siyo ya maoni ya CHADEMA au CCM au CUF au ya Warioba au Kikwete muache maneno wakati wa meneno umekwisha tunataka mkae na kazi ianze mwongozo upo na kilicho baki ni nyinyi sasa mkae hapo dodoma muanze kazi rasimu mko nayo na katiba ya zamani ipo tunataka mtuandike katiba ya  Watanzania ambayo itamlinda na kumpa haki yake MTanzania wa Bara na Visiwani awe kilema,mtoto,mzee,wa makamu,au kijana,katiba ambayo ina samini utamaduni wetu na kulinda mila zetu pamoja na kulinda mali zetu na ambayo itakuwa  mwongozo  wa uongozi wa kisiasa,kiuchumi,sheria,demokrasia,na accountability na responsibility na mwongozo elimu na health ,katiba itakayo mtowa au kumpa mwongozo wa kumtowa mtanzania kwenye umasikini.

NINGEPENDA KUMNUKUHU BABA WA TAIFA KIPENZI CHA WATANZANIA THE GREAT BLACK WA KARNE YA ISHIRINI ALIVYOSEMA PALE DODOMA WAPIGA KURA TUPATIHENI RAISI ANAYE FAA.  

NA MIMI NASEMA NYINYI WABUNGE WA CCM, WA CHADEMA,CUF,DP NA HAO WABUNGE WA VYAMA VINGINE NA VIONGOZI WENU TUNATAKA KATIBA YA WATANZANIA SIYO YA MAONI ,

WAKATI NI HUU NA MUDA NI HUU MTUPE KATIBA YA WATANZANIA NA SIYO YENU NYINYI MNAYOTAKA TUNATAKA KATIBA YA WATANZANIA, MWONGOZO MKO NAO.

 IT IS TIME, WE ARE  TIRED OF YOUR NOISE. 
IT'S  TIME YOU  WENT TO WORK .
Bwana michuzi asante  kwa kunipa 
nafasi ya kutowa maoni yangu

Yusef Israel

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. The mdudu,ww mdau hilo jina lako la mwisho ni tosha kabisa,mbona sijakupata point yako pasipo kutaja Tanganyika yangu huyu kuku wa muungano anaumwa sn dawa yake ni visu vitatu hop umenielewa?

    ReplyDelete
  2. Wasaliti wanaonekana. Tanzania maskani ya wasio na uzalendo.

    ReplyDelete
  3. Bwana michuzi huyu bwana yusef yuko wapi ameongea point kubwa sana hapa na huyu mdau wa kwanza anasema akuelewa ajuiu alicho sema huyu bwana yusef akupngelea mambo ya Zanzibar au Tanganyika ameongelea katiba ya Wa Tanzania anaangalia mbele na mbali aangalihi kwa kifupi nimesoma maoni yake ni mafupi lakini yana ujumbe mzito sana sana naomba bwana michuzi kamaunaweza kuhusukuma huu ujumbe wa huyu bwana yusef kwa waheshimiwa au kwenye blog zingine au kwenye Radio au magazeti bwana yusef tunashukuru kwa huu ujumbe

    Ndugu masoud.

    ReplyDelete
  4. Zanzibar na Tanganyika kwanza ndio Tanzania yenye amani itapatikana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...