Na Sylvester Onesmo
wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limeendelea kufanya msako katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata wanawake wapatao 15 wanaojihusisha na biashara haramu ya kuuza miili yao kutoka mikoa mbalimbali nchini. Msako huo ulifanyika tarehe 05/02/2014 majira ya 21:00hrs katika mitaa ya uhindini na Air Port.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi DAVID MISIME - SACP amewataja watu hao kuwa ni:
1. VERONICA D/O JOEL mwenye miaka 23, Mnyakyusa mkazi wa Sai Mbeya.
2. ROSE D/O MICHAEL mwenye miaka 30, Mgogo, Mkazi wa Kikuyu Dodoma.
3. MARIAM D/O JORDAN mwenye miaka 26, Mhehe mkazi wa Tukuyu Mbeya.
4. REHEMA D/O RAMANDANI mwenye miaka 38, Mlugulu makazi wa Airport Morogoro.
5. JOYCE D/O MARTINE mwenye miaka 22, Mnyamwezi mkazi wa Chinangali West Dodoma.
6. FATIA D/O SARATIELI mwenye miaka 20, Mgogo mkazi wa Makanda Bahi Dodoma.
7. BOKE D/O CHACHA mwenye miaka 27, Mkurya mkazi wa Tarime Mara.
8. SWAUMU D/O BAKARI mwenye miaka 23, Mnyamwezi mkazi Chinangali Dodoma.
9. ROSS D/O MASAKI mwenye miaka 28, Mchaga mkazi wa Sanya juu Moshi.
10. SCOLASTIA D/O COSTANTINO mwenye miaka 22, Mnyakyusa mkazi wa Gongolamboto Dar es salaam.
11. HAPPY D/O JULIUS mwenye miaka 31, Mnyamwezi mkazi wa Urambo Tabora.
12. AISHA D/O HASSAN mwenye miaka 38, Mbulu mkazi wa Babati Manyara.
13. JULIANA D/O DOMINICK Mwenye miaka 31, Mnyakyusa, mkazi wa Airport Dodoma.
14. DATIVA D/O LUKWEMBE mwenye miaka 29, Mhaya mkazi wa Kiziba Bukoba Kagera.
15. DORIN D/O MASSAWE mwenye miaka 23, Mchaga mkazi wa Kiboshomaro Moshi.
Aidha Kamanda MISIME amesema katika msako huo watu wawili wanaume walikamatwa wakiwa na mirungi robo kilo katika mtaa wa barabara ya nane (8) Manispaa ya Dodoma ambao ni NASSOR S/O ALLY mwenye miaka 45, Mwarabu mkazi wa barabara ya kumi na AYUBU S/O TEPO mwenye miaka 40, Muarusha, Fundi cherehani mkazi wa Chamwino.
Pia huko katika Wilaya ya Kongwa kijiji cha Mlanje kata ya Matongoro Tarafa ya Zoisa alikamatwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la SHEDRACK S/O MACHILE mwenye miaka 46, Mgogo, Mkulima akiwa na Lita 30 za pombe ya moshi akiziuza.
Kamanda MISIME amesema msako unaendelea na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.
vikundi vya kina mama na mashirika yasiyo ya kiserikali yawatafutie mtaji wakina mama hawa kama wanataka kuacha ukahaba. Wakati huu tunapoelekea kusherehekea siku ya wanawake hawa nao wachangiwe waache kujidhalilisha barabarani.
ReplyDeleteJe, kuna umuhimu wa kutaja makabila ya hawa makahaba?? Mimi naona kama kungetajwa majina yao tu na maeneo waliyokamatiwa inatosha. Naona in future, mtataja pia na dini zao
ReplyDeleteDu! pole za hawa kina dada! Alisema Mhubiri mmoja hapa nchini! Usione makahaba ukafikiri wanapenda au wanaamua kufanya hivi! Ni pepo tu ametawala mawazo ya akili zao. Wanahitaji ukombozi wa kiroho na kijamii.
ReplyDeleteSasa mkiwakamata mtawapeleka wapi? Na je mikoa mingine mnafanya hivi? Wanahitaji kwenda Rehab haouse!
The mdudu,hahahaaaaa mbavu zangu jamani mdau hapo juu kaguswa na hiyo kitu ya kuuza uroooda baada ya kuona KABILA LAKE WAKO WENGI mmmnoooo mdau usikonde hizo ni changamoto za maisha mabovu ijapokua mnajitapatapa mbelezetu eti oo sisiwajanja tuko juu haya sasa mmeumbuka mchana kweupe hongera sn ww kamanda wa polisi huko DODOMA wembe huohuo endelea kuwasaka na uwaanike hazarani kuanzia Majina mpaka MAKABILA YAO na mikoa yao wanakotoka,.mdau utaumia sn,hata mm niliposikia MLUGULU nilistuka sn ila nimeshukulu kuona yupo mmoja tu na tutamkanya ili aache hiyo tabia mbaya.pole sn mdau hapo juu.
ReplyDeleteHivi ni kweli haki kukamata wanawake pekee yao bila wanaume?! Kwani hawa wanwake wanafanya ngono pekee zao? Nadhani bila
ReplyDeletewateja hawa wadada hawana soko. lakini haki inapopotea upande mmoja unapoonewa basi hakuna haki. Naomba Polisi muliangalie hilo. Naelewa wengi wateja wa hawa madada wanaweza kuwa watu wakubwa Bungeni, basi vile vile msiwakamate hawa. La sivyo kamata na wabunge.
Majina ya kinababa waliokuwa wanannunua yako wapi? Ukahaba unatokana na pande zote, wauzaji na wanunuzi, tena ingependeza zaidi majina ya wanunuzi yangewekwa labda hii itapunguza huo ukahaba. Niliwahi kuishi mahali ambapo polisi walikuwa wananyang'any magari ya wanaonunua na kuwaambia wakayakomboe huko yalikutunzwa.
ReplyDeleteHii ya kutaja makabila imenikera sana, sijui Jeshi la Polisi lina interest gani kutaja makabila inapotokea tukio kama hili au ajali. Nadhani anapoishi, umri wake kazi yake vinatosha-iachwe aitwe Mtanzania au mkimbizi inatosha. La kama ajli au kifo, huenda dini yake vyaweza kuwekwkwa ili kufanikisha taratibu za mazishi kwa mujibu wa dini yake
ReplyDeleteAfadhali mhaya mmoja...naona makabila mliokuwa mnajidai sijuhi wacha Mungu sijuhi nini sasa mnaongoza kwa hii biahsara...te te tee
ReplyDeletePolisi muendelee kutaja makabila...mwendo mdundo