Mhe Profesa Mark Mwandosya akitoa neno la busara na kuweka mambo sawa kabla ya kuanza kwa mjadala leo jioni.
 Mjumbe  Mhe. James Mbatia akiongea kabla ya mjadala kuanza jioni hii
Ile sintofahamu iliyoibuka asubuhi wakati wa mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalum mjini Dodoma imekwisha na sasa Wajumbe wanaendelea kujadili kifungu kimoja baada ya kingine kwa amani, maelewano na busara.
Mwenyekiti wa muda Mhe Pandu Ameir Kificho alianza kuwatangazia wajumbe kwamba Wajumbe Mhe Christopher Ole Sendeka na Mhe
Abubakar Khamis Bakari wamemaliza tofauti zao na wote wawili wamerudi Bungeni wakiwa hawana kinyongo na kwamba  mshikemshike wa asubuhi ulikuwa ni moja ya changamoto za mijadala kama hiyo.
Mhe Kificho pia aliwakaribisha wajumbe Mhe Profesa Mark Mwandosya na Mhe. James Mbatia kusema machache kabla kuanza mjadala rasmi. Nao bila ajizi na kwa utulivu na maneno ya busara waliwataka wajumbe kukubali yaliyopita si ndwele na wagange yajayo.
Mhe Mbatia alimnukuu mmoja wa wajumbe wa kamati kama hiyo ya Ufaransa kwa kusema kuwa maridhiano na busara ndivyo viliwezesha nchi hiyo kujadili na hatimaye kuapata katiba yake.
Mhe Profesa Mwandosya alionesha imani kwa wajumbe wote kuwa na uwezo wa kuhitimisha kazi waliyotumwa na wananchi kwa maridhiano na kwa muda uliowekwa na kuokoa gharama.
"Niwahakikishie wananchi wa Tanzania kwamba hii kazi mliyotutuma tutaifanya na kuikamilisha kama ilivyokusudiwa", alkisema huku akishangiliwa.
Hivyo basi, hivi sasa mjadala unaendelea na wajumbe wamekubaliana mjadala huo wa kupitia Rasimu ya Kanuni zitakazotumika katika Bunge Maalum la Katiba unaendelea bila kelele wala mikwaruzo.
Hadi Mhe Kificho anaahirisha Semina hadi kesho saa nne kamili asubuhi, hakuna kokoro ingine iliyorekodiwa na kila mjumbe aliondoka kwenda kupumzika akiwa na furaha na fahari kwamba siku imemalizika vyema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...