Kikosi cha Kagera Sugar
Na Faustine Ruta,
Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea leo na hapa Mjini Bukoba tukishuhudia Timu ya Maafande kutoka Jijini Mbeya ikinyukwa bao 2-1 na wenyeji Kagera Sugar katika uwanja wa Kaitaba.
Kipindi cha kwanza Tanzania Prisons ndio walipata bao kupitia kwa mchezaji wao Peter Michael katika dakika ya 37 baada ya kuwachambua kama karanga mabeki wa Kagera Sugar na kuachia shuti kali na kumfunga kipa wa Kagera Sugar.
Mpaka dakika za mapumziko Tanzania Prisons ndio wameenda kupumzika wakiwa mbele ya Bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.Kipindi cha pili dakika ya 55 Kagera Sugar walipata penati na mkwaju huo ulipigwa na Salum Kanoni na kupata bao la kusawazisha.
Katika dakika za lala salama dakika ya 88 Kagera Sugar walipata bao la ushindi lililofungwa na Benjamini Asukire kwa shuti kali ndani ya eneo hatari la penati nakufanikisha Timu yao kuibuka na ushindi wa bao hizo mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...