Na Fakih Mapondela wa Tabora Police Press
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan S. Kaganda Alhamisi  tarehe 20/03/2014 alifanya ziara katika manispaa ya Tabora na kukutana na kikundi shirikishi (Sungusungu) na kukipatia mafunzo mbalimbali ya ulinzi shirikishi na ukamataji salama wa watuhumiwa pamoja na kukipa somo la dhana ya Polisi jamii.
Kamanda Kaganda akiwa katikati ya Sungusungu kuonesha mbinu bora za ukamataji salama wa watuhumiwa
Kamanda Kaganda akiwa katika harakati za kutoa somo la dhana ya polisi jamii
Hapa Kamanda Kaganda anajumuika kucheza ngoma na Sungusungu hao
Baada ya shamrashamra Sungusungu wote na wananchi wanakaa chini kumsikiliza Kamanda Kaganda
Wake kwa waume wakimsikiliza Kamanda Kaganda ambaye ameleta muamko mkubwa wa ulinzi shirikishi kwa wananchi wa mkoa wa Tabora
Juu na chini Kamanda Kaganda akihutubia wananchi wa mkoa wa Tabora ikiwa ni pamoja na mafunzo mbalimbali ya ulinzi shirikishi na ukamataji salama wa watuhumiwa pamoja na kukipa somo la dhana ya Polisi jamii.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Yaani Ulinzi Jamii hauwezi kukamilika mpaka Sungusungu waamshe Mizuka ya Wahenga kwa ngoma, tunguli na mavazi asilia!.

    Hayo ma-maski ya mabox hawa walinzi wajadi wanaweza kuona na kutekeleza majukumu kwa ufanisi kweli?

    Mdau
    Diaspora

    ReplyDelete
  2. wewe anony wa kwanza wala sio Diaspora, uwafanye wana-Diaspora kuwa wana akili finyu.

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Diaspora Usilewe Ugeni wa nchi hiyo uliyopo, usijifanye wewe si mtanzania, huku ndiko nyumbani, nchi aiwezi kupoteza utambulisho wake katika mambo ya kijamii, lipi ulilo litaka wewe,! wawe na vifaru???!!! si asili yetu. Tumesha kaa sana huko ulipo tunajua na wao uheshimu ya kwao. HONGERA KAMANDA S.
    Madau SIXMUND

    ReplyDelete
  4. Msela wa Tabora anavuta Ganja , swhuuuuuu(anavuta ndani moshi wa msuba), fwaaaaaa(anatoa nje moshi)!,

    Mwenzake anamuuliza hiyo Ganja ya wapi?

    Msela wa Tabora anajibu: Hii ya Mboka baba! (akimaanisha ya kuwa hii ni Bangi ya hapa hapa nyumbani Tabora)
    ................

    HAROO PALE MNAVUTA NINI HAPO? NAOMBA MUNIEREZE MIMI AFANDE SUZAN KAGANDA !
    ................

    Ohooo Masela wa Tabora acheni Bange Afande Suzan Kaganda atawafunga Jela!!!

    ReplyDelete
  5. Tabora acheni wizi wa ng'ombe na Kilimo cha Bange Afande Suzan Kaganda atawamalizia Kifungoni Magereza!!!

    ReplyDelete
  6. Kamanda nakukumbuka siku ile ulipofanikisha kuwatuliza watu za haki za binadamu walipokuwa wanataka kuandamana kwa sababu ya mgomo wa madaktari, Ulitumia diplomasia ya hali ya juu

    ReplyDelete
  7. Kamanda Kaganda nimekuaminia, hongera sana.

    Kamata uzi huo huo mama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...