Safari ya msafara wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula mwishoni mwa juma katika kukagua miradi inayofadhiliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na wahisani wengine katika Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa haikuwa rahisi kutokana na kukabiliwa na changamoto ya barabara kutokana na mvua kubwa kunyesha na hivyo kupelekea magari ya mizigo inayokwenda nchi jirani za Burundi na DRC kupitia bandari ya kasanga kukwama na kuziba njia. Juhudi za ziada kwa kushirikiana na wananchi pamoja na mkandarasi anaejenga barabara hiyo ya Sumbawanga - Kasanga kwa kiwango cha lami zilisaidia katika kuhakikisha magari yote yaliyokwama pamoja na msafara wa katibu Mkuu yanavuka salama.   
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Sulula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia).
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake wakikagua vitanda kwa ajili ya wanafunzi pamoja na daharia katika shule ya  Sekondari Kasanga  Mkoani Rukwa. Mradi huo wa daharia (bweni) ni kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika Shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake katika kukagua ujenzi wa miundombinu inayoendelea kujengwa katika soko la samaki la Kirando Wilayani Nkasi Mkaoni Rukwa mwishoni mwa juma.(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hiyo barabara hapo juu changamoto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...