Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola Comrade Julio Mateus Paulo akipokelewa na Ndg. Phares Magesa Mjumbe wa NEC kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipowasili leo. Katibu Mkuu huyo wa Chama kinachoongoza Angola amewasili Dar es Salaam  kuhudhuria Mkutano wa vyama vya Kisoshalisti ulimwenguni unaoanza kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
 Ndg.Magesa (MNEC) akiwa katika mazungumzo mafupi na Comrade Paulo katika ukumbi wa VIP uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola Ccomrade Julio Mateus Paulo akiongozana na  Ndg. Phares Magesa Mjumbe wa NEC kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwasili leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. CCM pia ni chama cha kisoshalisti?tuelimisheni jamani!

    ReplyDelete
  2. Ujamaa ni Utu, Utu, Utu!

    Ubepari ni Unyama!

    Hatuwezi kuishi kama wanyama ambapo nguvu za mmoja wapo zinategemea ukali wa makucha yake na ukali wa meno yake!

    Ngrrrrrrrrrrrr (Simba analia)
    ....................

    HIYO ILIKUWA NI UTANGULIZI WA TAARIFA YA HABARI KTK RADIO TANZANIA MIAKA HIYOOO KITAMBO YA SIASA YA UJAMAA.
    ....................

    Kama zilivyo nchi zingine za dunia kama Scandinavia zina mfumo wa Masoko huria na baadhi ya mielekeo ya Kibepari lakini wangali nao Ujamaa kiaina.

    Na ndivyo Tanzania ilivyo, ukiitazama utaoana ina Uchumi huria lakini Ujamaa ungalipo kimwelekeo kulingana na kuwa pana FAIDA na HASARA za kila kitu ikiwepo Siasa ya Ujamaa, ukitazama utaona kwa upande mmoja wa Sarafu ukiwa na mapungufu lakini upande wa Pili wa Sarafu Ujamaa umetusaidia KAMA TUTAVYOONA TULIVYO TOFAUTI NA JIRANI ZETU KENYA, UGANDA NA RWANDA.

    Ndio hapo sasa tunaona Makomredi wakiwasili kutokea Angola kuja Tanzania kwa ajili ya Kikao cha Ujamaa.

    Sasa tazameni ndugu zetu Madiaspora wanataka Pasipoti ya Pili na Uraia Pacha, HIVI NCHI YENYE VIASHIRIA VYA SIASA YA UJAMAA KAMA TANZANIA NA MASUALA YA URAIA PACHA WAPI NA WAPI?

    Madiaspora mnatwanga maji kwenye kinu, tungali na Ujamaa kimtindo hivyo sula lenu la Uraia Pacha Marijooo!

    ReplyDelete
  3. Kumbe ccm nacho ni chama cha kishoshalist ?

    ReplyDelete
  4. Mimi nilidhani kwenye usoshalisti tulishahama baada ya kunufaika na elimu bure na huduma nyingigine sasa tuko kwenye uchumi huru ambao siyo wa kikapitalisti au kisoshalisti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...