Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto),
akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa ofisini
kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la
Transaid la nchini Uingereza, hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika
viwanja vya NIT.
Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo
Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo
hicho. Magari hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza
Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya
kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na
Shirika la Transaid la nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini
Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi funguo za gari aina ya Iveco kwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva
yanayotolewa na Chuo Cha Taifa Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya
chuo hicho leo Asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya
kuinulia mizigo focal lift kama ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na
Shirika la Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT), leo asubuhi.
Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina
ya Folk Lift lililokabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya wanafunzi
wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo yamekabidhiwa leo asubuhi katika
viwanja vya Chuo hicho.
(Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Ni maoni tu.
ReplyDeleteJe security ya picha ya mwisho ikoje, je huyu kiongozi kweli anafahamu uendeshaji wa hii mashini au ndio balaa tuna karibisha? photo opportunity isije leta balaa, hapo pembeni kuna tenki, sijui maji au mali mlipuko...
tafadhali rekebisga lugha hii sio Gari ni kitendea kazi au mashine au nyenzo ya kubebea mizigi mizito. SIO GARI
ReplyDelete