Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera sana Dicota na TZ-Diaspora kwa kazi yenu kubwa mnayofanya katika harakati za uraia pacha. Tupo pamoja. Daima Mmbongo-Chiberia.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli tupo diaspora lakini kwa hoja kama hizi ambazo hazina mashiko bado hamjasimama sawasawa juu ya kuutetea huo uraia pacha.kumbukeni utanzania si kabila ambalo huwezi kulikana.utanzania ni utaifa ambao umewekewa kanuni zilizoanishwa kwenye katiba.kwa hiyo unaweza ukawa mchaga,mhaya au mbondei lakini si mtanzania kwa sababu ukiwa na akili zako timamu uliukana na kuchukua uraia wa nchi nyingine.kwa haki yako ambayo wana kijiwe mnasema mmepokonywa si kweli ila mmejipokonya wenyewe.sina maana ya kupinga hizo harakati za uraia pacha,la hasha ila nataka watetezi wake na hoja jadidi na zenye mashiko ila wakikaa kwenye majukwaa kama haya wawe na ushawishi kwa wanaowasikiliza.

    ReplyDelete
  3. Anon wa pili nakuunga mkono, pamoja na kwamba tulio wengi ugenini tungependa kupata uraia pacha ili kuendelea kutunza uzawa wetu(utanzania) nafikiri hoja hii imekosa nguvu na mwelekeo na nitashangaa sana kama itapita Bunge la katiba.

    Ugumu sio kwamba wajumbe hawataki kupitisha hii hoja, ugumu ni kwamba sisi kama wanachama wa diaspora pamoja na 'kusoma' tumeshindwa kujenga hoja ya msingi kwanini tupate uraia pacha. Mambo ya kwamba tunatuma hela kila mwaka kwahiyo tunachangia uchumi ni lame points: kwani utakataa kumtumia hela mama yako au mdogo wako eti kwa vile wewe sio raia wa Tanzania???

    Arafu sasa hivi mnataka tuanze kutoa michango ili kuwaonga wabunge, pleaseee

    ReplyDelete
  4. Kijiwe cha Ughaibuni ninakipenda sana kutokana na michango ya wachangiaji wake walivyo natural. Lakini kuna kitu ambacho nimekiona katika Wana-Diaspora wenzetu wa USA katika kuchangia Uraia pacha inakuwa kama vile wao ndiyo Wana-Diaspora zaidi kuliko wenzao walioko Europe, Asia, South America, Canada na nchi zingine za Ki-Afrika. Wanajisemea wao japo hata sisi tungepata access ya kuongea na chombo kama hicho tungetoa yetu ya moyoni.
    Kila wanachozungumza wao ni kuhusu Uraia wa Amerika na Tanzania.
    Kijiwe hiki tunajua kipo USA, lakini sidhani kama kimetayarishwa kwa Watanzania wenzetu walioko USA pekee, nadhani ni kwa Watanzania (Wana-Diaspora) wote.
    Najua nitaulizwa kutaja moja baada ya lingine malalamiko yangu. Mtu ukisikiliza midahalo yote hasa ihususuyo Uraia pacha utaelewa mara moja. Haina haja kuuliza.
    - Mr Mhoja - Sweden

    ReplyDelete
  5. mnapotoa comment katika hoja muhimu kama hii, jaribuni kuwa wastaarabu msikatishe watu tamaa ya kujadili mamboya msingi. watanzania daima tuimarishe usikivu na udadisi wa mambo ya maendeleo na sio chuki. mungu ibariki Tanzania na Watu Wake

    ReplyDelete
  6. I still think that they should emphasise "sisi USA Diaspora tunatake uraia pacha". They are the only ones making noise about it. They have the CCM branches etc, what else can you have - Is there no mechanisms in the party to advance this? Why the branches then? I live o/s and I personally do not want it and am sick of it. It helps me nothing.

    On top of that they have a rep in the Bunge, so I can't understand all these upumbafu.

    Go back home if you want to be a true Mwananchi.

    ReplyDelete
  7. Pamoja na kwamba mimi ni mwana-diaspora ila ni ukweli kwamba tumeshindwa kujenga hoja za msingi kwa nini tunataka uraia pacha, sitoshangaa kama ukikataliwa

    Binamu

    ReplyDelete
  8. Neno "Jadidi" kwa kiarabu lina maana ya Kipya, jipya hivyo nadhani ulitaka kusema "Shadidi" ambapo kwa kiarabu pia lina maana " Nzito"

    Hivyo ulitakiwa kutumia neno "Shadidi" katika maoni yako.(Mchangiaji wa 2)

    ReplyDelete
  9. Tuna hili dubwana linaloyumba na kwenda ali jojo linaitwa AFRIKA YA MASHARIKI.

    Nafikiri kwa kuwa sote ni ndugu na huko wameruhusu hiyo Dual Citizenship mngeomba Rwanda, Kenya na Uganda na sio Tanzania!

    ReplyDelete
  10. Si mlitaka chaiiiiiiiiiiii, mbona mnalalamika mnaunguaaaaaaaaaaa.

    ReplyDelete
  11. NI KWELI WALITAKA CHAI SASA WANASEMA YA MOTO WANATAKA IWE MAJI, HAWAJUI CHAI ILIKUWA MAJI KABLA YA KUWA CHAI HIVYO HAIWEZI KUWA MAJI TENA LABDA WAPEWE MAJI MENGINE NA HATUWEZI KUCHANGANYA NA CHAI KWANI ITAKUWA KITU KINGINE. TULIENI HUKO HUKO MKIJA BONGO MTAISHI KWA KIBALI/PERMIT HAPO MANZESE/TANDIKA KWA BABA YAKO MWALUGUSI, NA WEWE AMERIKA UNATUMIA SURNAME YA GUSSY KWA KUWA MWALUGUSI UNAONA NI USHAMBA ....TULIZENI KIPAGO.

    ReplyDelete
  12. Msiah yanabadilika sana duniani!

    Hamuwezi kuamini Watanzania walikuwa wanakwenda Malawi na Zambia kununua nguo na raba miaka ya 1980.

    Na sasa mambo yamebadilika Wazambai na Wamalawi wao ndio mwanakuja Tanzania kununua bidhaa na nguo tena bidhaa zenyewe ukiziona utacheka sana!,,,ni vyombo vya Plastiki kama

    -Mabirika ya Plastiki,
    -Mikeka ya Plastiki,
    -Viti vya Plastiki,
    -Mabegi ya Plastiki na makoro koro kibao ambayo hata wewe huwezi kubeba kuwapelekea Kijijini hapa TZ!

    Sasa ndio ndugu zetu Madiaspora wa Majuu walipigania juu chini kuondoka Tanzania wakafanikiwa tena wengine walifosi kwa kuwaacha watu na ndugu zao vibaya na sasa wanapigania kurudi Tanzania!

    Ndio vile Malawi na Zambia ilikuwa ni Majuu kwa Watanzania miaka ya 1980 na sasa 2014 Wamalawi na Wazambia WANAKANYAGANA KUJA TZ, KWAO MAJUU IMEGEUKA KUWA NI TANZANIA!

    ReplyDelete
  13. naona hoja zimelenga kwenye emotions na culture zaidi. swali tutafaidikaje na raia pacha?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...