Mwenyekiti wa Umoja wa Magereza Afrika, Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Afrika Kusini, Nontsikelelo Jolingana akitoa hoja ya kufungua rasmi Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014. Kikao hicho kimefanyika hivi karibuni Mwishoni mwa mwezi Februari, 2014 Nchini Afrika Kusini na kuhudhuliwa na Nchi Wanachama ikiwemo Tanzania.
Washiriki wa Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika wakiendelea na majadiliano ya Kikao hicho Jijini Johanesberg, Afrika Kusini hivi karibuni. Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao toka Nchi Wanachama Barani Afrika wakifuatilia kwa makini mjadala katika Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014.
Baadhi ya Wakuu wa Magereza Afrika wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga rasmi Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza wa Afrika unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014. Kikao hicho kimefanyika mwishoni mwa mwezi Februari 2014 Jijini Johanesberg Afrika Kusini(wa kwanza kushoto mstari wa mbele) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Afrika Kusini, Nontsikelelo Jolingana(wa kwanza kushoto mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Namibia, Raphael Hamunyela( wa pili kulia mstari wa mbele) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Msumbiji, Dkt. Eduardo Mussanhane (wa kwanza kulia mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja.
Sekretarieti Kuu ya Umoja wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Urekebishaji/Magereza Afrika mara baada ya kufungwa rasmi kwa Kikao cha Maandalizi ya Kikao cha Maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Magereza unaotarajiwa kufanyika Nchini Msumbiji Julai 2014(wa tatu toka kulia mstari wa nyuma) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wadau wa Lupango!

    Jamani tujitahidi kwa kuishi tukifuata sheria na taratibu, na pia tuombe yasitukute kama tunavyoona Wadau wana jipanga ili kuimarisha na kuwa uwezekano wa kuchomoka kwa kutoroka kama vile unazidi kubana.

    Maisha ya ndani ya Magereza hayana uzoefu!

    ReplyDelete
  2. Ohhh wanasema kuwaita,

    Wazee wa Lupango,!

    Wazee wa Mukenge,!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...