Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, Machi 26, mwaka huu, katika eneo la Kigamboni, wilayani Temeke akiwa katika ziara yake mkoani Dar es Salaam, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama. 


   Akizungumza na wananchi wa Kigamboni, Ndugu Kinana ameahidi kulichukua suala linaloonekana kuzua mgogoro mkubwa baina ya wananchi na serikali la ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigamboni,  na ameahidi kulifikisha kwenye vikao vya ngazi ya juu kabisa vya CCM kwa uamuzi wa uhakika na wa kudumu.
  Kinana amesema, baada ya kulifikisha kwenye vikao vya juu ya CCM atarejea tena Kigamboni kuzungumza na wananchi ili kuwapa majibu sahihi.
   "Hapa ni lazima tujue, wazo la kubuniwa mradi huu lilianzishwa na nani, kwa lengo na maslahi gani, na wananchi ninyi mnaoishi hapa mlihusishwa kwa kiwango gani kuhakikisha mchakato mzima unakuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi", alisema Kinana.

 
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana alipoowahurubia katia mkutano huo
 Kassim Abdallah mkazi wa Vijibweni Kigamboni akitoa hoja zake mbele ya Kinana kuhusu mradi huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kwenye kivuko pale kuvuka ni kero kama mtu ndiyo una gari yako ni kero mara mbili.wanatakiwa wajipange pantoni kubwa walau ziwe mbili.na tujue daraja limefikia wapi.serikali hii sikivu ifanye haraka daraja lianze tumechoka kukaa kwenye foleni ya kusubiri pantoni masaa 4 hiyo ni asubuhi bado jioni masaa mengine 4

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...