Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko amefunga tawi la Chadema katika Kijiji Cha Lukozi na kupandisha Bendera ya Chama Cha Mapinduzi kutangaza Ufalme mpya wa Chama hicho cha siasa.

Tukio hilo limetokea jana tarehe 6th March 2014 katika kijiji cha Lukozi, wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga, ambapo sambamba na kuasisi tawi hilo la Chama Cha Mapinduzi pia kiongozi huyo wa UVCCM ameingiza wanachama wapya 206 ambapo wengi wao walikuwa ni wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM, alifungua mashina sita yakiwemo ya Manyara, bodaboda, n.k pia alifanya vikao vinne vya ndani ambapo alizungumza na wanaCCM juu ya hali ya Uimara wa Chama na kuhoji kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Kijiji hicho ndani ya Wilaya ya Lushoto pamoja na kufanya mkutano wa hadhara ambao ulihudhuriwa na wananchi wengi wa Lukozi.

Pamoja na vikao hivyo lakini pia Husna alitembelea vikundi vya ujasiriamali vya  akinamama pamoja na kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto na kujadili nao Changamoto wanazokutana nao na kushirikiana nao kuzipatia ufumbuzi.

Husna anafanya ziara za kawaida katika Mkoa mzima wa Tanga katika kuhamasisha Vijana kujiunga na Chama Cha Mapinduzi pamoja na Jumuiya ya Umoja wa Vijana.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga,Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko akikabidhi kadi UVCCM kwa mmoja wa vijana wa kambi ya JUDO ya Vijana wilayani Lushoto.
jumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kutoka Mkoa wa Tanga,Ndugu Husna Mbwambo Sekiboko akipandisha bendera ya CCM kwenye moja ya mashina ya chama hicho.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hongera sana dada. Mwanzo mzuri!Junior Kimweri

    ReplyDelete
  2. Husna Mbwambo ni Jemadari wa Chama cha Mapinduzi!

    Kata mti panda mti!

    ReplyDelete
  3. Chadema Makao Makuu habari ndio hiyo Lushoto, Ukuta umeanguka !

    SHINA LA CHADEMA LIMEGEUKA KUWA LA CHAMA CHA MAPINDUZI!!!

    ReplyDelete
  4. Mghoshi Kyadema (Chadema), Lushoto Marijooo!

    Mbwaye tigende kusagula Kapelo na Fulana za CCM naho!

    ReplyDelete
  5. PIGA NYUNDO YA CHAMA CHA MAPINDUZI juu ya Tawi la CHADEMA LUSHOTO, Ng'oa Bendera ya Chadema pandisha ya CCM!

    CCM juuuuuu!

    ReplyDelete
  6. Chadema inazidi kuvunjika na kuzama Kaburini huko Lushoto-Tanga!

    Safari hii mtapata Kura 3 au zisizozidi 12 namba ya mwisho kwa viatu.

    Mtakataa Uchaguzi wa 2015 mkipata Kura sawa na NAMBA ZA VIATU?

    ReplyDelete
  7. Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa mmeona hiyo?

    Hii ni kata funua ya mwaka Chdm imepokea kutoka kwa CCM.

    Chama cha Chadema chavunjika jumla jumla Kijijini Kukozi-Lushoto, Tanga!!!

    Hii ni Funga kazi funiko la mwaka 2014 kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015!

    ReplyDelete
  8. Vijana wa CCM Kijijini Lukozi wameimarika Kichama na kimwili kwa JUDO sasa habari ndiyo hiyo Chadema leteni ubwege wenu mkatwe chembe za vifuani kwa mabandama ya shoto-kan kama Jet LI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...