Taasisi inayojishughulisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto wa kike inayojulikana kama KIVULINI ya jijini Mwanza imefanya semina kwa wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa hapo jana ulimwenguni kote.
Mdahalo huo uliyofanyika katika ukumbi wa Nyanza uliopo katikati ya jiji la Mwanza ilikuwa na lengo la kuelimisha jamii juu ya swala zima la kuzingatia usawa wa kijinsia ili uweze kuwa chachu ya maendeleo katika jamii husika. Mdahalo huo ulihudhuriwa na wageni mbalimbali toka ndani na nje ya jiji la Mwanza.
Mdahalo huo wa wazi ulikuwa na ujumbe maalum kwa kuelekeza majadiliano ya jinsi ya kuthamini mchango wa wanawake ili kuleta chachu ya maendeleo katika jamii. Huku ukiongozwa na kauli mbiu ya “Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia.”
Mkurugenzi wa Taasisi ya KIVULINI Bw. Ramadhan Masele kizungumza na wananchi kutoka jijini Mwanza juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia katika jamii wakati wa mdahalo wa maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani.
Muasisi wa asasi isiyo ya kiserikali ya KIVULINI Bi. Maimuna Kanyamala akieleza jambo wakati wa mdahalo wa wazi kwa wakazi wa jiji la Mwanza katika kuchochea usawa wa kijinsia kuleta mabadiliko katika jamii. Bi Maimuna aligusia swala zima la wanawake kuzichangamkia fursa zilizopo hasa swala la kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jamii katika harakati za kuleta mabadiliko.
Bi. Joyce Kiria mtangazaji na muongozaji wa kipindi cha kutetea haki za Wanawake, Wanawake Live kinachorushwa na kituo cha EATV akielezea jinsi waandishi wa habari wanavyoweza kuleta chachu za mabadiliko katika jamii kwa kutumia taaluma yao. Bi Joyce alisema kwamba waandishi wanapaswa kutumia weledi wao katika kueleza jamii umuhimu wa kuleta usawa wa kijinsia.
Baadhi ya washiriki wa Mdahalo Ulioandaliwa na KIVULINI kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani “Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...